Serikali yalenga kuimarisha usawa mapambano dhidi ya VVU

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene amepongeza Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika Mkakati wa kupambana na Ukimwi kama janga la kitaifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akihutubia wakati wa utoaji wa Taarifa ya Hali ya Ukimwi Duniani.(Picha na OWM).

Hayo yamesemwa Waziri na Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene jijini Dar es Saalam wakati wa uzinduzi wa taarifa ya hali ya Ukimwi Duniani yenye kauli mbiu inayosema "Ukosefu wa usawa wenye hatari kubwa" (Dangerous Inequalities).

“Serikali imedhamiria kuweka usawa wa kijografia usawa kimazingira usawa kati ya watoto na wakubwa na usawa wa kiuchumi ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma sawa ili wasiathirike na wale walio athirika wapate huduma za matibabu lakini pia huduma sawasawa kuhakikisha wanaendesha maisha yao,”amesema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima amesema, Tanzania imejitahidi kupunguza Ongezeko la Maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kila Mwaka kwa miaka kumi mfululizo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Taarifa Hali ya UKIMWI Duniani.

“Tanzania Imejitahidi kupunguza vifo vinavyosababishwa na UKIMWI na imekuwa ikifanya vizuri katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI,"amesema.

Post a Comment

0 Comments