Wageni wadakwa Riyadh wakijihusisha na utoaji mimba

NA DIRAMAKINI

WANAWAKE wawili kutoka nje ya nchi, ambao wanajihusika na kazi haramu ya utoaji mimba kinyume cha sheria, wametiwa hatiani Riyadh nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya ndani nchini Saudi Arabia, Idara ya Afya ya Riyad ilifafanua kuwa, kukamatwa kwa watu hao kulifanywa kwa ushirikiano na mamlaka ya usalama.

Ilibainika kuwa, wanawake hao wawili wahamiaji walikuwa wakifanya kazi hiyo ya utoaji mimba kinyume cha sheria katika nyumba ya makazi ya kukodi iliyopo Kusini mwa Riyadh.

Aidha, idara hiyo ilidokeza kuwa, utoaji mimba huo ulifanywa katika mazingira hatari na yasiyo na mahitaji vifaa vya afya.

Maafisa wa Idara ya Usaidizi wa Utekelezaji katika Idara ya Afya ya Riyadh, kwa kushirikiana na mamlaka ya usalama, walifanya ukaguzi katika jengo hilo la ghorofa na kuwakamata wanawake hao baada ya kufuatilia vitendo vyao haramu vinavyodaiwa kutishia usalama wa wagonjwa.
 
Msako hiyo ulifanikiwa baada ya mamlaka hiyo kwa ushirikiano na usaidizi wa karibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Afya huko Riyadh, Dkt.Hassan Al-Shahrani kufika eneo la tukio.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news