Wananchi Zanzibar wakijia juu Chama cha ACT-Wazalendo kwa tamko la kupinga uteuzi wa Mkurugenzi ZEC

NA DIRAMAKINI

IKIWA ni siku chache zimepita baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi kufanya teuzi mbalimbali katika muendelezo wa kuboresha utendaji katika Serikali na vyombo vyake, wananchi na viongozi wa kisiasa visiwani humo wamejitokeza mbele ya waandishi wakitoa maoni na pongezi kwa uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),Thabit Idarous Faina.
Hayo yanakuja baada ya Chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo kujitokeza hadharani na kutoa tamko kwa kile ilichodai, Faina hafai kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

"Sisi TLP tumepokea uteuzi wa Mhe.Faina kama Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kuwa ni sahihi, katika chaguzi zote kumekuwa na wakurugenzi mbalimbali ila kwa Faina amekuwa mkurugenzi sahihi zaidi, hivyo tumefurahishwa na kurejeshwa kwake katika nafasi hiyo, mtu yoyote anayepinga uteuzi wa ndugu Faina basi itakua haeleweki popote,"amesema Hussein Juma Salum, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha TLP Zanzibar.

Nao baadhi ya wananchi wametumia fursa hiyo kuwaeleza waandishi wa habari na umma kuwa, teuzi hizi ni muendelezo wa mabadiliko chanya ndani ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt.Hussein Mwinyi ambapo pia wamempongeza na kumtia moyo Rais Mwinyi katika utendaji wake.

"Kiukweli tunafurahishwa na namna Dkt.Mwinyi anafanya kazi zake ikiwa ni pamoja na kubadilisha anapoona utendaji hauendi vizuri na kuacha pale penye ufanisi zaidi, kiukweli asife moyo sisi wananchi tuko nyuma yake yeye pamoja na mkewe mama Mariam,"amefafanua Faudhia Magome mwananchi mkaazi wa Zanzibar.

Nae Katibu Mkuu wa Chama cha upinzani cha Demokrasia Makini Taifa,Ameir Hassan Ameir ameeleza kutofurahishwa na kitendo cha ACT-Wazalendo kukiuka misingi ya Kikatiba ya kumtaka Mhe. Rais asitekeleze majukumu yake ya Kikatiba ya Uteuzi na Utenguzi kama ambavyo Katiba na Sheria za nchi zinamtaka kufanya hivyo.

Ndugu Ameir ameenda mbali na kutoa wito kwa wanasiasa wengine kuwa mstari wa mbele katika kustawisha demokrasia ya Zanzibar na si kuiwekea vizingiti, ambapo amedai iwapo ACT-Wazalendo walikua na hoja za jinai dhidi ya ndugu Faina mteuliwa wa nafasi ya Ukurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), basi walipaswa kutoa malalamiko na kesi yao kipindi hicho na si sasa wakati na mahali ambapo nchi imetulia na siasa zinakwenda vizuri.

"Pamoja na tamko hili la ACT-Wazalendo, walipaswa watoke hadharani kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2020 na watamke kuwa ni ndugu Faina ndiye aliyeleta fitna katika uchaguzi, ila hawakufanya hivyo na hii inathibitisha kuwa tuhuma hizi za uharamia katika uchaguzi wa 2020 si za kweli, sasa badala yake wanajitokeza sasa hivi kusema hivyo dhidi ya uteuzi halali na wa kisheria ambao Mhe.Rais ameufanya kwa mamlaka aliyonayo kikatiba;

Post a Comment

0 Comments