Waziri Simbachawene ampongeza mama Tunu Pinda

NA MWANDISHI WETU

"KUIMBA kuna nguvu kubwa; kuimba ni kusali mara mbili, wenzetu mmekuwa watumishi wa Mungu kwa njia ya uimbaji na kazi mnayoifanya ya utume inawasaidia mpate neema na baraka kubwa;
Mama Tunu Pinda (kulia) ambaye ni miongoni mwa Wanakwaya wa Mtakatifu Theresia Mtoto Yesu wakiimba mbele ya mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mtakatifu Theresia, Mtoto Yesu. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mtakatifu Theresia, Mtoto Yesu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Mtakatifu Theresia, Mtoto wa Yesu inayoitwa Mungu Asiyeshindwa iliyofanyika katika Parokia ya Nzinje mjini Dodoma.
Mama Mbonimpaye Mpango, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza jambo wakati wa Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mtakatifu Theresia, Mtoto wa Yesu.

“Kwaya hii ya Mtakatifu Theresia, Mtoto Yesu ndio anayoimbia Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda, amechagua jambo zuri sana la kufanya baada ya kustaafu,”amesema Waziri Simbachawene.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akimkabidhi kanda ya nyimbo (CD)Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda.

Post a Comment

0 Comments