Fedha za Mfuko wa Jimbo kuendelea kuchangia ujenzi wa maabara za sekondari Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

KATIKA kuendelea kuboresha sekta ya elimu hasa kwa masomo ya Sayansi katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara fedha shilingi milioni 75 za mfuko wa jimbo zilizopokelewa hivi karibuni zitachangia ujenzi wa maabara tatu katika baadhi ya shule za sekondari jimboni humo.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 21, 2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo.

"Ni sekondari tatu tu zenye maabara tatu, Physics, Chemistry na Biology zilizokamilika na zinatumika ipasavyo. Sekondari nyingine zinatumia vyumba vya madarasa kuwa maabara zao zinapohitajika.

"Kwa hiyo shilingi milioni 75 za mfuko wa jimbo zilizopokelewa hivi karibuni zitatumika kuchangia ujenzi wa maabara hizo tatu kwenye baadhi ya sekondari zetu. Sekondari zinazohitaji kuchangiwa vifaa vya ujenzi vya maabara zao, zinaelekezwa kutuma maombi kwa Katibu wa Kamati ya Fedha za Mfuko wa Jimbo...Afisa Mipango wa Halmashauri yetu kabla ya tarehe 10, Januari 2023.

"Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Sekondari 27, ambapo zote zitachukua wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2023. Jimbo la Musoma Vijijini lina kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374. Jumla ya Shule za Msingi jimboni ni 118, shule tatu ni za binafsi vilevile tunazo shule shikizi nne kati ya sekondari hizi 27, Sekondari za binafsi ni mbili, na za Serikali/Kata ni 25,"imefafanua taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, baadhi ya kata zimeamua kujenga sekondari nyingine zaidi ili kutatua matatizo ya umbali mrefu wa wanafunzi wanaoutembea kwenda masomoni, na vilevile kutatua tatizo la msongamano wa wanafunzi madarasani. Sekondari mpya tano zimepangwa kujengwa, na ujenzi umeanza kwa baadhi ya kata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news