MNEC Dkt.Mabula awauma sikio viongozi wa CCM

NA MUNIR SHEMWETA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula amewataka viongozi wa chama hicho Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam kuhakikisha viwanja vya chama hicho vinatambulika kisheria kwa kuwa na hatimiliki ili kuepuka uvamizi au kuibiwa maeneo ya chama.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam alipotembelea ofisi za chama hicho Desemba 20,2022. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Rogert Mbowe.

Dkt.Mabula amesema hayo Desemba 20, 2022 wilayani Ubungo mkoani Dar es Salaam alipotembelea ofisi za CCM wilayani humo kwa lengo la kusalimia ikiwa ni siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo, Rogart Mbowe (kulia) akizungumza wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula alipotembelea ofisi za chama hicho zilizopo Kibamba mkoani Dar es Salaam tarehe 20 Desemba 2022.

"Ni lazima chama kisimame kiuchumi kwa kuhakikisha viwanja vitambulika kisheria kwa kuwa na hatimiliki na kama kuna nafasi chama kiweke mipango vizuri ikiwemo ya ubia,"amesema.

Kwa mujibu wa Dkt.Mabula, CCM inavyo viwanja vingi kwenye maeneo mbalimbali nchini, lakini baadhi yake haviko kisheria ingawa vinatambulika kama mali ya chama na kubainisha kuwa kutotambulika kisheria kumepitwa na wakati na kikubwa ni kujua namna uendelezaji rasilimali za chama unavyofanyika.
"Kama kuna viwanja basi iwekwe mipango vizuri na ikiwezekana kuingia ubia na taasisi kwa ajili ya kuendekeza, lazima tuangalie maeneo yaliyo katika 'prime area'. Tusiwe na mawazo tu kuwa hizi ni mali za CCM,"amesema Dkt.Mabula.

Aidha, Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa alikipongeza Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ubungo kwa kuwa na eneo lake Kibamba Dar es Salaam na kufanikiwa kujenga ofisi ya chama ambapo aliuelezea uamuzi huo kuwa, unakisaidia chama kuepukana na utaratibu wa kupangisha ofisi.

Amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo kufanya kazi kwa bidii na kuishauri serikali kutimiza majukumu yake ambapo alisisitiza kuwa hayo yote yakitimizwa basi wataweza kuiunganisha serikali na chama na kuongea lugha moja.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula akivishwa skafu na vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo alipotembelea ofisi za chama hicho.

"Kubwa tufanye kazi kwa bidii na kuishauri serikali na kikubwa kutimiza majukumu kupitia ngazi mbalimbali za chama kuanzia shina na tukiweza kuyasimamia hayo ni jambo la msingi na tutakuwa tumeunganisha chama na serikali vizuri na tutakuwa tunaongea lugha moja, kikubwa kuhakikisha utekelezaji wa ilani kama ilivyokusudiwa,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news