Ubungo wamsikitisha Waziri Dkt.Mabula

NA MUNIR SHEMWETA

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ameonesha kutorishwa na kasi ya wananchi wa Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam kutochangamkia fursa ya kupatiwa hati kupitia zoezi la urasimishaji makazi holela.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akimkabidhi hati mkazi wa wWlaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa zoezi la utoaji hati kwa wananchi wa wilaya hiyo waliokamilisha taratibu za kupatiwa hati katika zoezi la urasimishaji makazi holela Desemba 20,2022.
Hali hiyo imejitoleza wakati wa utoaji hati miliki za ardhi kwa wananchi 1081 wa maeneo tofauti wilayani Ubungo waliokamilisha taratibu za kumilikishwa ardhi kupitia zoezi la urasimishaji makazi holela Desemba 20, 2022 eneo la Stop Over Kata ya Saranga Dar es Salaam.

Huku akieleza kupitia takwimu za zoezi la urasimishaji katika Wilaya ya Ubungo, Dkt. Mabula amesema kazi kubwa imefanywa na ofisi ya ardhi Halmashauri ya Ubungo ambapo hati miliki 1081 zimekamilishwa na kugawiwa kati ya viwanja 23,967 vilivyopimwa na kuidhimishwa.
"Wote waliotimiza wajibu wao hakuna hati inayodaiwa hapa. Wapo waliotimiza wajibu na hawaendi kuchukua sasa unataka serilali ifanye nini? alihoji Waziri wa Ardhi Dkt. Angeline Mabula.

Kwa mujibu wa Dkt.Mabula, changamoto ya zoezi urasimishaji makazi holela ipo pande zote mbili za wananchi na makampuni yanayofanya kazi za urasimishaji na kusema kuwa haiwezekani hati 1081 pekee ndiyo zikamilishwe na kugawiwa wananchi kati ya viwanja 23967 vilivyoidhinishwa.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa zoezi la utoaji hati kwa wananchi wa wilaya hiyo waliokamilisha taratibu za kupatiwa hati katika zoezi la urasimishaji makazi holela Desemba 20,2022.

"Haiwezekani Ubungo idadi ya vipande vya ardhi vilivyotambuliwa ni 182, 215 kutoka michoro 520. Idadi ya vowanja vilivyopangwa na kuidhinishwa ni 177,325. Idadi ya viwanja vilivyowekewa bicon 76,250. Vilivyopimwa na kuidhinishwa ni 23,967. Ankara zilizotoka 4338, idadi ya maombi ya hati 7164, idadi ya hati zilizotolewa 6,885 na leo kuna hati 1,081 ukijumlisha hapo maana yake hakuna hati inayodaiwa katika ofisi ya ardhi,"amesema Dkt.Mabula.

Amesema, kwa wale wote waliotimiza wajibu wao hakuna hati inayodaiwa mpaka wanakwenda kutekeleza zoezi la kugawa hati wilayani Ubungo, lakini wapo wale wananchi waliotimiza wajibu wa kulipa na kuandaliwa hati lakini hawaendi kuchukua na kuhoji hapo serikali ifanye nini na kunainisha kuwa ilichoamua wizara yake ni kuwafuata walipo kwa lengo ni kuhakikisha hakuma wanachodai ndani ya wizara.Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibamba Issa Mtemvu pamoja na kuelezea kuendelea vizuri kwa zoezi la urasimishaji makazi holela kwa baadhi ya kata za jimbo lake na kuzitaja Saranga, Ukombozi na Mpakani, lakini baadhi ya wananchi wanakabiliwa na changamoto za malipo ya kukamilisha ili kupatiwa hati na kuiomba wizara kuangalia namna ya kuwasaidia ili waweze kupatiwa hati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news