Rais Dkt.Mwinyi:Serikali imedhamiria kutumia mifumo ya kisasa kukusanya mapato

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali imejipanga kutumia mifumo ya kisasa ya ukusanyaji mapato ambayo itarahisisha kulipa kodi kwa wakati na kuongeza mapato ya nchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Tuzo ya Mlipa Kodi Mkubwa wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Bw.Actaf Jiwan wa Kampuni ya Zanzibar Petroleum Ltd, wengine ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt.Saada Mkuya Salum na Kamishna wa ZRB,Yussuf J.Mwenda,hafla ya maadhimisho ya kusherehekea Kilele cha mwezi wa Shukrani na Furaha kwa Walipakodi kwa mwaka 2021/2022 imeyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, Desemba 29, 2022. (Picha na Ikulu).

Amesema, katika kufanikisha hatua hiyo, serikali imedhamiria kuibadilisha Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na kuwa Mamkala ya Mapato Zanzibar (ZRA) ili kuenda sambamba na malengo ya Serikali yaliyojiwekea katika kuwafikishia maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Desemba 29, 2022 kwenye maadhimisho ya siku ya shukurani na furaha kwa walipakodi Zanzibar, huko ukumbi wa Golden Tulipo, Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.
Amesema, lengo la kuundwa kwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar, siyo kupandisha kodi kwa walipa kodi, bali ni kutumia wigo mpana wa kuzidisha ukusanyaji wa mapato kwa njia za kisasa utakao kwenda sambamba na mifumo ya kiteknolojia ambayo itawarahishishia walipa kodi na sio kutumia nguvu kubwa kwa walipa kodi.

“lli Serikali ikusanye mapato zaidi mbali ya kuwa na mamlaka, lakini kuwa karibu zaidi na walipakodi bila kutumia nguvu kwa walipa kodi wake, ili wafanyabiashara walipe kodi stahiki,”amefafanua Rais Dkt.Mwinyi.
Rais Dkt.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwashauri wananchi na wafanyabiashara kuendelea kujenga utamaduni wa kudai risiti wanapofanya manunuzi ya bidhaa ama huduma, sambamba na kuwasihi wafanyabiasha kutoa risiti mara baada ya kutoa huduma kwa wananchi.

“Kutokudai risiti wakati wa kufanya manunuzi ni kuwanufaisha wachahce kwa sababu kodi ikibaki kwa mfanyabiasahara itamnufaisha yeye na sio Serikali,”amefafanua Rais Dkt. Mwinyi.

Akiwazungumzia wanaohujumu mfumo wa ulipaji kodi, Rais Dkt.Mwinyi amebainisha kwamba, serikali haitasita kumchukulia hatua ofisa masuuli yeyote aliyepewa jukumu la kuzuia mapato na kutokuyafikisha kwa wakati.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Tuzo Maalumu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum na Kamishna wa ZRB,Yussuf J.Mwenda, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Kilele cha mwezi wa Shukrani na Furaha kwa Walipakodi Zanzibar kwa mwaka 2021/2022, Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

Hata hivyo, Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza Mamlaka ya Mapato ZRB kwa kuanzisha wazo la mwezi wa shukurani na furaha kwa walipakodi na kushauri kuwa wazo hilo liwe endelevu kila mwaka ili kujenga uwelewa mpana na kutoa hamasa kwa wananchi kulipa kodi kwa wakati.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt.Saada Mkuya alisema mafaniko ya ukusanyaji wa mapato ZRB ni mafanikio yaliyofikiwa na kuboreshwa kwa mifumo mipya ya ukusanyaji kodi kwenye taasisi hiyo.

Amesema, nia ya kuibadilisha Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na kuwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ilikuja baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kupitishwa muswada wa Sheria Disemba 14 mwaka huu na kueleza kuwa lengo la mabadiliko hayo ni kuifanya Zanzibar kuwa na mapato yenye tija zaidi na kuifanya taasisi hiyo iwe na mtazamo chanya wa ukusanyaji wa mapato yake.

“Lazima utendaji ubadilike, ZRB iwe taasisi inayoaminika zaidi” alikazia Waziri Mkuya.

Naye Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Yussuf Juma Mwenda amesema, ZBR ina lengo la kuongeza makusanyo ya kodi ili kufikia asilimia 100 ya makusanyo hadi mwezi Juni 2023 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo alieleza wanatarajia kukusanya shilingi bilioni 579.
Amesema, hadi mwezi Novemba mwaka huu ZRB ilifanikiwa kukusanya shilingi 238.5 bilioni na kueleza kuwa imefikia ufanisi wa asilimia 91 ya makusanyo yanayofanywa na taasisi hiyo ambayo kwa sasa alieleza imekuwa kwa asilimia 67.5

Pia amesema, mafanikio hayo yanatokana na ufanisi wa ZRB chini ya usimamizi mzuri wa Waziri wa Fedha sambamba na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa kodi kwa ushirikiano mkubwa wa Serikali mtandao aliouelezea kwamba unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja na kuongeza kuwa mfumo huo utaanza kutumika rasmi mwezi Januari, mwakani.

Ameongeza kuwa, ZRB imeadhimisha siku ya shukurani kwa walipakodi Zanzibar kutokana na ushirikiano mkubwa walioupata baina yao na kueleza kuwa katika kuifanikisha siku hiyo walifanikiwa kuwafuata walipa kodi na kusikiliza changamoto zinazowakabili za masuala ya ulipaji kodi na kuzitatua.

Mwenda amesema, walifanikiwa kuwafikia walipakodi 442 pamoja na kuwatembelea wafanyabiasha 456 kwa lengo wa kuwasikiliza walipakodi hao na kuongeza kuwa ZRB ilifanikiwa kuzifikia kaya 100 kwenye kijiji cha Kangagani Pemba pamoja Kiojini Matemwe, mkoa wa Kaskazini Unguja kwa lengo la kuwapatia misaada ya kijamii sambamba na kuendelea kuhamasisha ulipaji kodi na kudai risiti za kielektroniki.
Katika maadhimisho ya siku ya shukurani na furaha kwa walipa kodi Zanzibar kuliambatana na sherehe za ugawaji wa tunzo kwa walipa kodi waliochangia zaidi pato la taifa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo makundi manne muhimu yaliwania tunzo hizo wakiwemo Walipa kodi wakubwa kwa Unguja na Pemba.

Jumla yao Kamisha Mwenda aliwataja ni 187 ambao walifanikiwa kukusanya kodi zaidi ya asilimia 65 kwa Unguja na Pemba, ikilinganishwa na walipa kodi wote, Kundi la walipa kodi kwa mikoa mitano ya Zanzibar ambao waligawa kwenye vipengele vya walipa kodi wanaowajibika, kwa kulipakodi kwa wakati, kutoa risiti bila ya kusukumwa, kurejesha marejesho ya kodi kwa wakati na rekodi zao kwenye risiti zao hazipunguzi wala kuzidisha.

 Aidha, kundi lingine lililopokea tunzo hizo ni Walipakodi wakubwa na Walipa kodi wanaotumia mfumo wa risiti za kielektoroniki. 

Zanzibar Petrtolium Ltd aliibuka mshindi wa Mlipakodi bora kwa mwaka wa Fedha, 2021/2022, ambapo tunzo yake ilipokelewa na Altaf Jiwan, mwakilishi mkaazi, Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news