Rais Dkt.Mwinyi:Serikali itaendelea kuweka mkazo uboreshaji Sekta ya Afya

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa,Serikali itaendelea kuweka mkazo uboreshaji wa Sekta ya Afya nchini.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Desemba 21, 2022 kwenye mahafali ya 20 ya Chuo Kikuu cha Zanzibar yaliyofanyika Tunguu Wilaya ya Kati katika Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema, Sekta ya Afya ina mambo mengi ambayo yanahitajika kufanywa ikiwemo kupitia upya sera za afya na mifumo yake.
Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alisema kuwa, hatua hiyo ni msingi mzuri wa kuharakisha mageuzi katika sekta hiyo muhimu nchini.

Amesema, tofauti na miaka ya nyuma, Zanzibar ilikuwa na watumishi wachache ikilichangishwa na sasa ambapo kuna wataalamu wengi na mabingwa katika fani mbalimbali za tiba.
Katika maelekezo yake Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema, wataalamu hao wengi wao wamepata elimu nchini.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amekipongeza Chuo Kikuu cha Zanzibar kwa kuanzisha kozi ya shahada ya sayansi katika Afya ya Jamii huku akionekana kufarijika zaidi kutokana na chuo hicho kuanzisha programu nyingi za uzamili hususani katika fani ya afya na sayansi shirikishi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum na Mkuu wa Chuo Kikuu Zanzibar (Zanzibar University),Mhandisi Dkt.Abulqadir Othman Hafiz, baada ya kumalizika kwa Mahafali ya 20 ya Chuo hicho yaliyofanyika Desemba 21,2022, katika viwanja vya Chuo Kibele Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news