Rais wa UAE, Amir wa Qatar wajadiliana mambo muhimu

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani wamekutana na kujadiliana kuhusu uhusiano wa kindugu na njia za kuimarisha ushirikiano wao ili kuendeleza maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili.

Hayo yalikuwa ni sehemu ya mazungumzo yao rasmi yaliyofanyika Desemba 5, 2022 katika Ukumbi wa Emiri Diwan huko Doha, Qatar.

Amiri wa Qatar alimkaribisha Rais wa UAE na kumpongeza kwa mnasaba wa kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya 51 ya UAE, na kuitakia UAE na watu wake kuendelea na maendeleo na ustawi chini ya uongozi wa Sheikh Mohamed.

Pia alielezea matumaini yake kuwa ziara hiyo itaimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Qatar, hivyo kusaidia kupanua mipango thabiti waliyonayo kwa ustawi bora wa pande mbili.

Rais wa UAE alirejea pongezi zake kwa Sheikh Tamim na wananchi wa Qatar kwa mafanikio makubwa ya kuandaa Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) 2022 na kueleza kuwa ni jambo la fahari kwa nchi zote za Baraza la Ushirikiano la Ghuba, na kwa ulimwengu wa Kiarabu kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, mafanikio ya Qatar katika kuandaa mashindano hayo ya kimataifa ya michezo ni dhihirisho la uwezo wa watu wa nchi za GCC na ulimwengu wa Kiarabu katika kuandaa matukio ya kimataifa kwa ubora na ufanisi mkubwa.

Rais wa UAE alitoa shukrani zake na pongezi kwa Amir wa Qatar kwa mapokezi mazuri na ukarimu alioonesha kwake na ujumbe wa UAE.

Mkutano huo uliangazia uhusiano wa UAE-Qatar na matarajio ya kukuza ushirikiano wao ili kuimarisha ustawi katika nchi zote mbili na kutumikia maslahi yao ya pamoja katika maeneo ya kiuchumi, uwekezaji na biashara.

Sheikh Mohamed na Sheikh Tamim pia walijadili umuhimu wa kuboresha mfumo wa kazi wa pamoja wa GCC ili kuhudumia maslahi ya watu wao na matarajio yao kuelekea maendeleo zaidi na ustawi mkubwa.

Pia walipitia masuala kadhaa ya kuheshimiana, na kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya kikanda na kimataifa. (WAM)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news