Wadakwa kwa kukutwa na vifaa vya mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji mkoani Pwani limesema linawashikilia watuhumiwa 65 kwa makosa mbalimbali wakiwemo wahalifu waliokamatwa na vifaa vya mradi wa umeme katika Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji,ACP Protas Mutayoba amebainisha hayo leo Desemba 7, 2022.

ACP Mutayoba amesema kuwa,jeshi hilo liliendesha operesheni kali katika mkoa huo na kufanikiwa kukamata mtungi wa gesi uliokuwa unakwenda katika Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.

Pia amesema kuwa, jeshi hilo limefanikiwa kukamata watuhumiwa wa dawa za kulevya na pikipiki zinazotumika katika matukio ya uhalifu.

Katika tukio lingine Kamanda Mutayoba amesema, jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa kosa la kukutwa na nyara za serkali na mitego ya kutegea wanyama. Ambapo amebainisha upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Maisha kwa hatua zaidi.

Sambamba na hilo Mutayoba ameeleza kuwa, jeshi hilo liliendesha operesheni ya usalama barabarani ambapo makosa 4085 yalirekodiwa kutokana na makosa mbalimbali.

ACP Mutayoba ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi hilo ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahalifu hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news