IJP WAMBURA AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kwenye mikoa mitatu.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 6, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo, IJP Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Muslim kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Alex Mukama ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

IJP Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

Aidha, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shadrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news