Magazeti leo Juni 19,2026

Serikali imeendelea kuimarisha hatua za kuzuia ugonjwa wa Ebola kuingia nchini huku ikithibitisha kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa aliyegundulika Tanzania, licha ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda.
‎Akizungumza na waandishi wa habari Juni 18,2026 jijini Dodoma , Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema mifumo ya ufuatiliaji, utambuzi na udhibiti wa ugonjwa huo imeimarishwa ili kuhakikisha usalama wa afya za Watanzania unaendelea kulindwa wakati wote.

Amesema Serikali ilichukua hatua za mapema mara baada ya kutangazwa kwa mlipuko huo katika nchi jirani, ikiwemo kutoa Mwongozo wa Wasafiri Na. 17 wa Mei 19, 2026, unaobainisha tahadhari na masharti ya kiafya kwa wasafiri wote wanaoingia nchini.
“Tunaendelea kuwafahamisha wananchi kuwa hadi sasa nchi yetu haina mgonjwa wa Ebola na hali ya usalama wa afya nchini iko vizuri. Serikali imejipanga kikamilifu kuzuia, kugundua mapema na kudhibiti tishio lolote la ugonjwa huo,” amesema Mchengerwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here