NA JOHN MAPEPELE
VIONGOZI wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo wakiongozwa na Mheshimiwa Waziri Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi leo wameshiriki kwenye onesho la Mario.

Onesho hilo la muziki lijulikanalo kama 'The Kid You Know' limefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mamia ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya wamefurika kushuhudia tukio hili la kihistoria.

Mgeni rasmi kwenye tukio hili ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.Wasanii mbalimbali pia wamemsindikiza Marioo katika shoo yake na kupamba tukio hili.