Nyasa kuanza msako wa wanafunzi nyumba kwa nyumba

NA DIRAMAKINI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imefanya kikao cha tathimini ya walioripoti na kuanza elimu ya awali na darasa la kwanza katika shule za msingi na kidato cha kwanza katika shule za sekondari wilayani Nyasa.

Kikao hicho kimefanyika Januari 19, 2023 katika Ukumbi wa Kapteni John Komba, Mjini Mbamba bay na kuwakutanisha viongozi wa Vijiji,Kata, Wakuu wa Idara na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa. Mgeni Rasmi katika kikao hicho ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Aziza Mangosongo Akifungua kikao, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema, lengo la kikao ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kwenda sekondari, na waliohitimu umri wa kuanza elimu ya awali na darasa la kwanza wanaanza na kuacha visingizio.

Amewataka viongozi wa vijiji, kata na halmashauri kwa ujumla kuendesha msako wa nyumba hadi nyumba na kutowaachia walimu peke yao. Amefafanua kuwa, Viongozi hawa ndio wanaoishi na jamii na kuwafahamu wakazi wao, na kujua kuna watoto wanaotakiwa kwenda shule.

“Ninyi Viongozi wa Vijiji na kata yaani Watendaji wa Vijiji, na Kata mnaishi na wananchi na mnawafahamu wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza, na waliotimia Umri wa Kuanza darasa la Awali na la kwanza Wilayani Nyasa, hivyo tunatakiwa kuhamasisha jamii kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakwenda shule.

Mh.Mangosongo amempongeza Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa Kuipa miradi ujenzi wa Madarasa Wilaya ya Nyasa na kutatua kero za miundombinu ya elimu.

Awali Wakitoa Taarifa ya wanafunzi walioripoti na kuanza masomo katika Shule ya Msingi, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Mwl Hossein Mghewa amesema Wanafunzi walioanza masomo ni asilimia 101 kwa darasa la Awali na Asilimia 102 kwa darasa la kwanza hivyo Amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa, bado wanaendelea na uhamasishaji, lengo ni kuhakikisha kuwa wanavuka lengo kwa asilimia nyingi.

Akiwakilisha taarifa ya Elimu Sekondari Kaimu Mkuu Divisheni ya Elimu ya Sekondari, Mwalimu Aus Limia amesema, asilimia 44 ya wanafunzi ndio walioanza masomo ya kidato cha kwanza hadi kufikia Januari 18,2023. Kikao kimeazimia kufanyika kwa uhamasishaji na elimu kupitia vikao vya WDC na Vijiji na kuanza msako wa nyumba hadi nyumba na kuhakikisha wanafunzi wote ndani ya wiki mbili wawe wameripoti shuleni kwa asilimia 100.

Kwa upande wake viongozi wa vijiji na kata wamemhakikishi Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kufanya msako na kuhakikisha wanafunzi hao wanaenda shule na zoezi hili kuwa endelevu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news