Prof.Muhongo aja na mkakati kabambe wa kuboresha Sekta ya Elimu jimboni

NA FRESHA KINASA

KATIKA kuendelea kubooresha Sekta ya Elimu, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo anatarajia kuendesha harambee mbili kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika shule za sekondari mbili jimboni humo.

Hayo yamebaimishwa leo Januari 17, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ambapo taarifa hiyo imesema kuwa harambee ya kwanza itafanyika Bwai Sekondari tarehe 19 Januari, 2023 saa 9:00 alasiri.

"Bwai Sekondari, hii ni sekondari ya pili na mpya ya Kata ya Kiriba ambayo imefunguliwa wiki iliyopita mategemeo ni kuwa na wanafunzi 150 wa kidato cha kwanza. Harambee huko Bwai Sekondari itafanyika Alhamisi ya Januari 19,2023 saa 9:00 alasiri (15 hrs). Michango ipelekwe kwa Mkuu wa shule (Headmaster) 0757471516/ 0612409257.

"Harambee ya pili itafanyika Muhoji Sekondari, Januari 24,2023 majira ya saa 8:00 mchana, Muhoji Sekondari inajengwa kwenye Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne ambayo ni kubwa (eneo) kuzidi kata zote ambayo itakuwa ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema.

"Harambee ya Muhoji Sekondari ni Jumanne ya Januari 24,2023 saa 8:00 mchana (14 hrs). Michango ipelekwe kwa Mtendaji wa Kijiji (VEO) 0686557264.

"Michango inaombwa kwa wazaliwa wa Musoma Vijijini na hasa wa kutoka maeneo yenye miradi hiyo na wadau wengine wa maendeleo karibuni sana,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa.

"Jimbo la Musoma Vijijini lina kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374. Jimbo hili lina jumla ya Sekondari 27, ambapo shule 25 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi SDA na KATOLIKI. Tunaendelea na ujenzi na uboreshaji wa miundombimu iliyopungufu kwenye sekondari zetu za kata. Bado kuna mahitaji ya maabara, maktaba, vyumba vya madarasa, ofisi za walimu (majengo ya utawala), vyoo, nyumba za walimu, n.k. kwenye Sekondari zetu za kata,"imesema taarifa hiyo.

"Vilevile, kuna matatizo ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda masomoni, na mirundikano ya wanafunzi madarasani (wingi wa watoto wanaopaswa kwenda sekondari)-tunalazimika kuongeza idadi ya sekondari kwenye baadhi ya kata zetu.

"Tunashukuru sana Serikali yetu, chini ya uongozi wa Rais wetu, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombimu iliyotajwa hapo juu,"imesema taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news