Serikali yachoshwa na tabia za abiria kupigwa mawe ndani ya treni Kisumu

KISUMU-Maafisa wa Shirika la Reli nchini Kenya (KRC) na usalama wametoa onyo kali kwa wakazi wa Kaunti ya Kisumu nchini Kenya kutokana na kuongezeka kwa visa vya abiria kupigwa mawe.

Matukio hayo yamewasukuma wanausalama kufanya msako mkali huku wakifanya mkutano na wakaazi wa kaunti hiyo wanaoishi kando ya reli kuanzia eneo la Muhoroni hadi Kisumu mjini kuwaelezea kuhusu kadhia hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Reli na Bandari, Patrick Tito na Mkuu wa DCI wa Bandari na Reli, John Muinde waliwaambia wakaazi hao kuwa, visa hivyo havitapuuzwa tana.

Viongozi hao walisema kuwa, wana taarifa muhimu zinazowahusu watuhumiwa na kutoa wito kwa umma kushirikiana nao kwa karibu ili kuhakikisha wahusika wanachukulia hatua kali.

Aidha, Jeshi la Polisi wametaja visa hivyo, visivyokubalika na ambavyo haviwezi kuvumilika kwani kupitia uhalifu huo mara tatu katika maeneo ya Kibigori na Kandege huko Muhoroni vioo vya treni vilipasuliwa kwa kurushwa mawe na wahalifu hao.

Kamanda Tito alisema kuwa, uharibifu wa miundomisingi wa reli ni hatia kisheria na mhusika anaweza hata kuhukumiwa kifo akiwataka wakaazi kuwa tayari kulinda reli hiyo kwa ustawi bora wa miundombinu ya umma. (Tuko)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news