Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo yampa faraja Dkt.Kikwete kwa kuendelea kukuza vipaji

NA JOHN MAPEPELE

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho ameipongeza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kutokana kufanya vizuri kwenye Sanaa ya Muziki na Sanaa ya Filamu hapa nchini.
Mhe.Dkt.Kikwete amesema hayo wakati akitoa hotuba yake usiku wa kuamkia leo Januari 29, 2023 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa albamu ya 'The Kid You Know' ya msanii maarufu nchini Mario.
Amefafanua kuwa, ili sanaa iweze kukua hapa nchini inategemea mahitaji ya Serikali ambapo ametoa wito kwa Serikali kuendelea kulea sanaa.
Amepongeza Wizara kwa kufanikisha kuwa na mdundo ambao utalitambulisha Taifa la Tanzania duniani.

Pia amepongeza kwa Serikali kuanzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa na kuanza kutoa mikopo isiyo na riba na kuomba kuwa na mkakati madhubuti ambao utasaidia sanaa kwenye kwenye ngazi za kimataifa.
Tukio hilo limehudhuriwa na mamia ya wapenzi wa muziki huku wasanii mbalimbali wa nyimbo za kizazi kipya wakimsindikiza Marioo katika uzinduzi wa album hiyo.

Pia Katibu Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi na viongozi wengine pamoja na wadau mbalimbali wa muziki wamejitokeza

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news