DC wa Malinyi aagiza msako kwa wanafunzi 187 katika vituo vya bodaboda, michezo ya kubahatisha na mitaani

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, Mheshimiwa Sebastian Muungano Waryuba ameagiza kusakwa wanafunzi 187 ambao hawajaripoti shuleni kufikia Februari 14, mwaka huu.
Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wakuu wa taasisi za umma pamoja na wakuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ikiwa ni mkutano wake wa kazi na watumishi hao.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkuu wa divisheni ya elimu sekondari wilaya ya Malinyi Pendo Masalu wanafunzi187 kati ya wanafunzi 2,559 ambao wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza bado hawajaripoti shule.
Mkuu wa wilaya ameagiza vyombo vyote vya usalama vilivyopo wilayani humo kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Malinyi kuwasaka wanafunzi ambao hawajaripoti.

Amesema, wazazi wa wanafunzi hao wakamatwe na walazimishwe kuwapeleka watoto shule. "Nakuagiza mkuu wa divisheni ya elimu sekondari pamoja na maafisa watendaji kata na vijiji maafisa tarafa na vyombo vyote vya ulinzi muwasake hawa watoto na nipate taarifa wamesharipoti shuleni,"amesema.
Mbali na kuwasaka wazazi na wanafunzi hao ametoa maelekezo wanafunzi kusaidia shughuli za nyumbani siku za mwisho mwa Juma ambapo hakuna shughuli za masomo.

Kutokana na kasumba ya wanafunzi kuacha masomo na kwenda kufanya kazi ya bodaboda mkuu huyo wa wilaya ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya msako kukamata watoto walio chini ya miaka 18 wanaoendesha bodaboda.
"Na sio bodaboda nataka mfanye msako na katika michezo ya kubahatisha maarufu kama bonanza na pooltable sitaki kuona watoto walio chini ya miaka 18 katika michezo hiyo,"alisema.
Kuhusu suala la lishe na chakula mashuleni mkuu wa wilaya ya Malinyi amewataka viongozi kushirikiana kutoa elimu kwa wazazi ili wahamasike kuchangia chakula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news