Huyu hapa Padri Severine Msemwa aliyebeba kumbukizi kubwa ya ndoa ya Hayati Rais Dkt.Magufuli na Mama Janeth Magufuli

NA DIRAMAKINI

MKE wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, Mama Janeth Magufuli ameshiriki katika ibada ya kumbukumbu ya siku aliyofariki aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi huko Korogwe mkoani Tanga.
Balozi Kijazi alifariki dunia Jumatano ya Februari 17, 2021 saa 3 usiku katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mama Janeth Magufuli aliambatana na Mke wa Balozi Kijazi, Mama Fransisca Kijazi pamoja na familia wakiwemo viongozi wa dini.

Wakati huo huo, akiwa bado Korogwe, Mama Janeth Magufuli amekutana na Padri Severine Msemwa aliyewafungisha ndoa yeye na Hayati Magufuli miaka 33 iliyopita katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Wakati wa uhai wake, Hayati Rais Dkt.Magufuli aliwahi kusema kwamba, alifunga ndoa bila kuvaa koti la suti na mkewe Janeth hakuvaa gauni la bibi harusi.

Ndoa hiyo ilifungwa wakati Magufuli akiwa mwanafunzi katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na haikuambatana na sherehe yoyote.

Akiongea katika mdahalo uliofanyika UDSM kutathmini miaka mitatu ya uongozi wake wa nchi, Magufuli alisema alifurahi kurudi chuoni hapo ambapo si tu alipata elimu yake ya juu bali kufunga pingu za maisha.

"Siku niliyooa watu wengi hawakujua na haimaanishi sikuwa na pesa ya kununua koti au gauni la harusi kwa mke wangu, sikuona kama vitu hivyo ni vya msingi sana.

"Tulienda hapo kanisani pete tukanunuliwa na Padri, tena zilikuwa za shaba. Padre pia alitununulia soda, nakumbuka mimi nilikunywa pepsi na mke wangu alikunywa mirinda.Baada ya hapo nikaenda zangu lab (maabara) kuendelea na shughuli zangu,"alikaririwa Hayati Rais Dkt.Magufuli.

Padre ambaye aliwafungisha ndoa hiyo na kutoa ufadhili wa pete na soda kwa mujibu wa Rais Magufuli anaitwa Msemwa na sasa yupo Tanga. "Mfuateni father (Padri) Msemwa yeye atawaeleza vizuri zaidi."

Katika hatua nyingine, wakati huo Magufuli pia alisema hata ndoa za watoto wake huwa haziambatani na sherehe kubwa, "mpaka sasa watoto zangu watatu wameshafunga ndoa na sikufanya sherehe kubwa. Mmoja alifunga ndoa tayari nikiwa madarakani, lakini wala hamkusikia."

Rais Dkt.Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 61 kwa maradhi ya moyo.
Msgr. Severine Msemwa

Parents:
Father: Severine Joseph Kakiwa
Mother: Dominica Severine Njovu

Date and Place of Birth:
Date: July 1947, Village: Peramiho
Ward: Peramiho, District: Songea
Region: Ruvuma, Country: Tanzania


Deaconate and Priesthood
Deaconate: 26/06/1974
Priesthood: 29/06/1975


EDUCATION:
1954 – 1961 Primary Education- Kwagunda, Kilole and Kwediboma

1963 – 1965 Minor Seminary- St. Peter’s Bagamoyo
1966 – 1969 Junior Seminary St. Peter’s Bagamoyo and Itaga Tabora
1970 – 1972 Philosophical Studies – Kibosho Major Seminary
1972 – 1975 Theological Studies – Kipalapala Senior Seminary.
1977 – 1978 Diploma in Education, Chang’ombe TTC – DSM
1997 – 2000 BSC Human Service- Elmira College New York US.
2000 – 2002 MSC. Adult Education- Elmira College New York US.

OTHER COURSES AND ACHIEVEMENT:
August 2005 – Semina ya Ushauri Nasaha kwa Waathirika wa VVU Teule Hospital
November 1996 – Computer Literacy- University of Dar Es Salaam
November 2000 – Sexual Misconduct Policy Workshop, Diocese of Rochester USA
1973 – 1986 Librarian - Kipalapala, Ntungamo, TAPRI, St. Peter and Soni Seminary

WORKING EXPERIENCE:

1986 – 1989 Teaching, Ntungamo Major Seminary Bukoba
1989 – 1990 Teaching, Segerea Senior Seminary DSM
1990 – 1997 Chaplain, University of DSM
1997 – 2002 Assisting Priest St. Casimir’s Parish- Elmira New York, USA
2002 – 2004 Rector Soni SeminaryTanga Diocese
2004 - 2014: Parish Priest Potwe Parish Tanga
2014 -2017: Parish Priest at Mkuzi Parish, Lushoto.
2017 - Present: Chaplain COLU Sisters Kwamndolwa


CONTACT

Kwamndolwa Sisters Convent Chaplaincy
P.O. Box 280
Korogwe, Tanzania.
Phone: +255784334540
E-mail: mhangileki@yahoo.com

catholic diocese of Tanga

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news