Rais Dkt.Mwinyi afanya tena ziara ya kushtukiza kwa wafanyabiashara

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza mfanyabiashara wa bidhaa za vyakula katika Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, Bw.Seif Khamis Ali, alipofanya ziara ya kushtukiza leo Februari 18,2023 kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiangalia mchele wa Mbeya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo na kuzungumza na Mfayabishara wa Bidhaa za Vyakula katika marikiti hiyo, Bw.Seif Khamis Ali na kushoto kwa Rais ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi na kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kusalimiana na watalii waliotembelea Marikiti Kuu ya Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kutembelea Wafanyabishara ya vyakula katika Marikiti Kuu Darajani Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Mfanyabishara wa Nyama ya Ng’ombe katika Soko la Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja leo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Marikiti hiyo kuangalia hali ya bidhaa ya vyakula.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akilipia nyama ya ng’ombe baada ya kuinunua kwa Bw.Ali Hashim mmoja wa wafanyabiashara katika Marikiti Kuu Darajani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo na kushoto kwa Rais ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news