Waziri Balozi Dkt.Chana atua Kawe

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Februari 18, 2023 amefanya ziara katika eneo litakalojengwa viwanja kwa ajili ya michezo ya ndani lililopo Kawe Dar es Salaam, ambalo litatumika katika michezo ya kuogelea, masumbwi, mpira wa netiboli, wavu pamoja na matamasha mbalimbali.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Pindi Chana akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Said Yakub na Watendaji wengine wa Wizara hiyoleo Februari 18, 2023 Kawe Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika eneo la Ekari 12 litakalojengwa viwanja vya michezo mbalimbali pamoja na matamasha (Sports and Arts Arena).

Mhe. Pindi Chana ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa eneo hilo lenye ukubwa wa Ekari 12, ambapo likikamilika litakua na uwezo wa kuchukua watu takriban 16, 000 kwa wakati mmoja.

Waziri Chana amewataka Watendaji wa Wizara kuhakikisha michakato yote inayotakiwa inakamilika mapema ili ujenzi uanze na kukamilika kwa wakati. Mhe. Dkt. Chana aliongozana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Ally Mayay, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ununuzi Bw. Masubo Masubo, Mhasibu Mkuu Bw. Deogratias Mbinga pamoja na Maafisa wengine wa wizara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news