Serikali yaondoa ukomo Kitambulisho cha Taifa, hizi hapa faida

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Hamad Masauni amesema wamefanya mabadiliko ya kanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho vya Taifa.

Mheshimiwa Masauni ametoa kauli hiyo Februari 21, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na hali ya utolewaji wa vitambulisho.

Amesema, marekebisho ya kanuni yamekamilika na zimeshaanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi katika gazeti la Serikali la Februari 17, 2023.

"Nitoe rai kwa watoa huduma kwa wananchi hasa taasisi za kifedha, benki na kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo uliopita kwa sababu havitakuwa na ukomo tena wa matumizi.

"Marekebisho hayo hayahusiani na vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na kwamba muda wa vitambulisho hivyo uzingatiwe,"amesema Waziri Masauni.

FAHAMU MATUMIZI MAPANA YA KITAMBULISHO CHA TAIFA

Ewe Mwananchi, sasa unaweza kutumia Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN)/Kitambulisho cha Taifa (NID) kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama :-

  1. Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration),
  2. Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN),
  3. Kusajili Biashara/Kampuni – BRELA,
  4. Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport),
  5. Kukata Leseni ya Udereva,
  6. Kupata Huduma ya Afya,
  7. Kufungua Akaunti ya Benki,
  8. Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi za Fedha,
  9. Kujiunga na Elimu Ngazi Mbalimbali,
  10. Kupata Mkopo wa Elimu ya Juu,
  11. Hati Miliki ya Kiwanja, Nyumba n.k,
  12. Kujidhamini na Kudhamini Wengine,
  13. Kitambulisho cha Taifa kutokana na kuwa na Kisilikoni (Cheap) kinaweza Kutumika kama Pochi ya Fedha ya Kielektroniki (E-Wallet) ambako unahifadhi fedha na kufanya malipo kwa kutumia Kitambulisho Chako,
  14. Kitambulisho kinaweza kutumika kama ATM CARD,
  15. Kwenye Maingio ya Malango Kielektroniki (E-Entrace),
  16. Daftari la Mahudhurio la Kielektroniki (Electronic Attendance),
  17. Mwananchi kuondokana na Adha ya Kubeba Utitiri wa Vitambulisho kwani sasa taarifa zote Muhimu za mwananchi zitapatikana katika Mfumo Mkuu wa Taifa wa Utambuzi wa Watu,
  18. Kinaweza kutumika kama hati ya Utambuzi wa Utaifa wa wananchi wanaovuka mipaka ndani ya nchi zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.
  19. Vitaimarisha Utendaji Kazi Serikalini kwa Kuwa na Kumbukumbu Sahihi za Watumishi na Malipo ya Stahili zao, hasa Wanapostahafu,
  20. Kupata Ruzuku za Pembejeo za Kilimo Kirahisi,
  21. Kujisajili kwenye Chama cha Ushirika (Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Makundi mengine),
  22. Kupata Msaada wa TASAF unaotolewa kwa Kaya Masikini,
  23. Kufungua Akaunti za Benki,
  24. Kuomba Ajira pamoja na Huduma Nyingine Nyingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news