Spika Dkt.Tulia afanya mabadiliko ya kamati za kudumu za kisekta

NA DIRAMAKINI

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amefanya mabadiliko ya kamati za kudumu za sekta kwa kuunda na kuongeza idadi ya kamati kutoka tisa hadi 11 kwa sasa.

Mheshimiwa David Kihenzile ambaye ni Mwenyekiti wa Bunge ameyabainisha hayo Februari 6, 2023 katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.

Kihenzile amezitaja kamati hizo kuwa ni Ardhi, Maliasili na Utalii, Afya na Masuala ya Ukimwi, Nishati na Madini, Miundombinu,Utawala, Katiba na Sheria, Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Maji na Mazingira, Elimu, Utamaduni na Michezo.

Kamati zingine zisizo za kisekta zitaendelea kubakia kama awali ikiwemo Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Hesabu za Serikali (PAC), Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) na Bajeti.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 135 ambayo inaweka ukomo kwa kamati za Bunge mwisho wa mkutano wa 10 ambao nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge, wabunge wote wanatakiwa kujaza fomu za kujiunga na kamati za Bunge kwa kipindi cha pili cha Bunge,”amesema Mheshimiwa Kihenzuke.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news