TUSIMEZEE UOVU

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wametakiwa kuyasema mazuri ya wenzao na kuachana na tabia ya kusambaza mabaya kwa kuwa Mungu anayafahamu mazuri na mabaya ya kila mmoja wetu, kama angesambaza mabaya hali ya maisha ya mwanadamu ingekuwaje?,
Hayo yamesemwa na Padri Paul Mapalala Jumapili ya saba ya mwaka A wa Liturjia katika Kanisa la Bikira Maria Imekulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Februari 19, 2023.

“Sisi wanadamu tunasambaza mabaya ya mtu, tunakatazwa hilo, tujitahidi kuwa wakamilifu kama Baba yetu aliye Mbinguni, injili ya leo inatusogeza zaidi katika mapendo, inatuonya katika kutangazana mabaya. Kama una shida na mtu nenda kaongea naye yaishe, ndiyo maana tumepewa amri ngapi za Mungu?.

"Amri ngapi? Kumi, na yote yanazungumzia hayo hayo. Hilo halina maana wewe umezee uozo wa mtu, hapana nenda kazungumze naye, ‘Bwana unachokifanya siyo sahihi na siyo kizuri, fanya kama baba yetu wa mbinguni alivyo mkamilifu.’ Jamani hayo ndiyo tunayopewa katika masomo yote matatu ya leo, tusibaguane, tupendane, tushauriane, tuheshimiane, tushikane mikono ili twende sote mbinguni.”

Misa hiyo ya kwanza inayoanza saa 12.00 ya Asubuhi ya kila Jumapili iliambatana na mombi kadhaa yaliyotanguliwa na mwongozo huu,

“Kristo alituagiza tuwe wakamilifu kama Mungu alivyo mkamilifu, agizo lake ni la ajabu sana lakini sisi ni watoto Mungu lazima tuwe na tabia za Kimungu,” Eee Bwana twakuomba sikiliza maombi yetu.“Utusaidia tuwakubali watu wote kama ndugu na kushirikiana bila ubaguzi, dharau au chuki.” Hili likiwa ombi la kwanza.

Katika misa hiyo kwaya ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chamwino ambayo ni shule ya umma ya bweni inayokusanya vijana wa Kitanzania kutoa maeneo mbali ya taifa letu iliimba.

Mkusanyiko huo wa vijana kutoka kona zote za taifa hili ulijidhihirisha kutokana na nyimbo zote walizoimba tangu mwanzo misa hadi mwisho zilifahamika na waamini wote akiwamo mwandishi wa ripoti hii.
Hali ya hewa ya Chamwino Ikulu imekuwa ya jua kali mno kwa juma zima huku mahindi na mazao mengine kipindi cha mchana yamekuwa yakinyongonyea sana unapoyatazama kutokana na miale ya jua kuyashumbulia bila huruma lakini matumaini huonekana wakati wa Asubuhi na Jioni huku wakulima wakiwa na matumaini ya pili ya mvua kunyesha siku chache kuanzia Jumatatu ya Februari 20, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news