WAZIRI DKT. MABULA ATAKA MOTISHA OFISI ZINAZOFANYA VIZURI MAKUSANYO YA ARDHI

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Dkt.Angeline Mabula ametaka kuandaliwa utaratibu utakaotoa motisha kwa ofisi za ardhi zitakazofanya vizuri katika ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi ili kuleta ushindani.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt.Angeline Mabula akizungumza katika kikao kazi kati ya Menejimenti ya Wizara ya Ardhi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kilichofanyika taehe 16 Februari 2023 Morogoro. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Dkt.Allan Kijazi na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Musa Ally Musa.

Aidha, ametaka ofisi za ardhi katika mikoa na halmashauri nchini kuhakikisha zinatumia fursa ya Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi uliotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha wananchi wanaodaiwa kulipa kodi hiyo katika muda uliotolewa.
Sehemu ya Washiriki wa Kikao Kazi cha Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kilichofanyika tarehe 16 Februari 2023 Morogoro.
Sehemu ya Washiriki wa Kikao Kazi cha Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kilichofanyika tarehe 16 Februari 2023 Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi kwa wadaiwa kulipa deni la msingi kufikia Aprili 30, 2023.

Dkt.Mabula amesema hayo tarehe 16 Februari 2023 mkoani Morogoro katika kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa katika maandalizi ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2023/2024.

‘’Ni vizuri katika kuhamasisha ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi tukaangalia namna bora ya kutoa motisha kwa zile ofisi za ardhi zinazofanya vizuri, hii itasaidia kuongeza mapato,’’ alisema Dkt.Mabula.
Kamishna wa Ardhi Methew Nhonge (Kulia), Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Hamdouny Mansoor (katikati) na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Wolter Lungu wakiwa kwenye Kikao Kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kilichofanyika tarehe 16 Februari 2023 .

Akigeukia Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi uliotolewa na mhe. Rais Dkt Mabula alisema anataka kuona kila mkoa 'unachacharika’ kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kuhamasisha watu kulipa kodi.

‘’Nataka kuona kila mkoa unachaharika maana ni aibu msamaha unatolewa halafu tunakusanya kidogo, tutumie fursa ya msamaha wa Rais kuhamasisha wananchi na taasisi kulipa kodi ya pango la ardhi,’’ alisema Dkt. Mabula.

Aidha, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitumia fursa ya kikao kazi cha Wizara kutaka kuona malengo ya ukusanyaji mapato ya kodi ya ardhi yanakuwa na uhalisia badala ya kujiwekea malengo makubwa anayokinzana na hali halisi.

‘’Malengo yetu ya ukusanyaji mapato ya ardhi walau yasiwe yanakinzana na uhalisia kwa kujipa matumaini ya kukusanya kiasi kikubwa wakati uhalisia ni kukusanya kidogo,’’ alisema Dkt. Mabula.

Waziri Dkt.Mabula pia alielezea suala la Kliniki za Ardhi ambapo ametaka kupatiwa taarifa ya mikoa iliyotokeleza kazi hiyo kwa muda gani kutokana na kazi hiyo kuonesha kulegalega huku akibainisha kuwa, Kliniki hizo za Ardhi zinasaidia sana kutatua migogoro ya ardhi.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza katika Kikao Kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kilichofanyika tarehe 16 Februari 2023 Morogoro.

Kliniki za Ardhi ni utaratibu ulioanzishwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo kila mkoa unakuwa na Kituo Jumuishi kwa siku maalum na kutoa huduma mbalimbali za sekta ya ardhi pamoja na kusikiliza kero za wananchi .

Pia Waziri Dkt.Mabula aliagiza Wakurugenzi wa Wizara yake kutoka kwenda kwenye mikoa kuona kazi za idara husika zinavvyofanyika kwa lengo la kufahamu changamoto zilizopo na kusisitiza kuwa, utaratibu huo kutumika katika ngazi za mikoa kushuka chini na kubainisha kuwa bila kufanya hivyo kazi hazitafanyika kwa ukamilifu.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao kazi kati ya Menejimenti ya Wizara ya Ardhi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa tarehe kilichofanyika taehe 16 Februari 2023 Morogoro. (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE WIZARA YA ARDHI).

Katika kuhitimisha maagizo yake katika kikao hicho, Dkt.Mabula ametaka ushirikiano wa ofisi za ardhi za mikoa na zile za halamashauri kwa kutekeleza yale waliyokubaliana na kuwataka watendaji kutosubiri kuitwa katika matatizo na kusisitiza kutumia vikao kutoa ushauri kwa halmashauri.

Kikao Kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kinafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 15-17 Februari 2023 mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine kinajadili Bajati ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2023/2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news