Asasi za Kiraia Zanzibar (CSOs) zatakiwa kujitathimini

NA DIRAMAKINI

ASASI za Kiraia Zanzibar (CSOs) zimetakiwa kujiwekea utaratibu maalumu wa kujipima kila baada ya kipindi cha miezi mitatu kwa lengo la kujitathmini na kutambua njia bora za kufikia malengo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar, Dkt.Mzuri Issa wakati alipokua akizungumza na baadhi ya wawakilishi wa asasi 30 kutoka Unguja na Pemba katika mkutano uliofanyika kwenye umbi wa chama hicho Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.

Alisema, asasi za kiraia zina mchango mkubwa wakuleta mabadiliko kwenye jamii, hivyo wana wajibu wa kujiewekea utaratibu maalumu ambao utawapa fursa wahusika kujitathmini na kujua wapi walipo na wanataka kufanya nini.

Alisema, ili Asasi hizo ziweze kuendelea kufanya kazi zao kwa maslahi ya jamii wanapaswa kuacha kufanya kazi kwa mazoea wakiamini kuwa kila kitu ni rahisi na wataweza tu kutimiza wajibu wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mwavuli wa Asasi za Kiraia Zanzibar (ANGOZA),Hassan Khamis Juma alisema mkutano huo ni muhimu sana katika kupata taarifa za awali zinazohusiana na maswala ya utetezi ambazo,zitapelekea kujua mapungufu yaliopo hatimae kuchukuliwa hatua za kujengeana uwezo kukabiliana na mapungufu hayo.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo kujikita zaidi katika mambo muhimu ambayo yataorodheshwa na kisha kujadiliana kwa pamoja ili walio mwengi zaidi waweze kufaidika.

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo Maulid Sleiman kutoka (ZYF) alisema mkutano huo ni muhimu sana kwa maslahi ya Asasi na jamii kwa ujumla.

Alisema kukutanishwa pamoja kwa Asasi kunatengeza mahusiano mazuri sambamba na kujifunza kile ambacho wengine wanatekeleza na kuamini kuwa ni jambo muhimu sana.

Nae Zawadi Abdalla Khamis kutoka taasisi ya (ZGC) alisema mkutano huo utatoa mwanga na kutambua madhaifu yao kama wawakilishi wa taasisi zao na ndio njia kuu itakayopelekea mabadiliko.

Mkutano huo wa siku moja umeitishwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na shirika la Foundation for Civil Society.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news