Iddi Pialali na Mfaume Mfaume kuzichapa Septemba Mosi

NA DIRAMAKINI

MABONDIA Iddi Pialali na Mfaume Mfaume wamesaini mkataba kwa ajili ya pambano lao litalalofanyika Septemba 1, mwaka huu.

Akizungumza Promota wa Pambano hilo ambaye ni Mkurugenzi Poshy Queen Boxing Promotion Hamis Mrisho amesema kwamba pambano hilo litafanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Amesema kwamba kusainiwa kwa mkataba huo ni ishara kwamba pambano hilo lipo.
“Kusainiwa kwa mkataba huu inamanisha pambano lipo na litafanyika Septemba 1, 2023 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,” amesema Mrisho.

Mrisho ameabainisha kuwa pambano hilo ni lakushindania mkanda wa WBF International, kwamba mshindi ataondoka na mkanda huo.

Kwa upande weka Mfaume amewahakishia wapenzi wa ngumi na mashabiki wake kwamba pambano hilo lipo na wasahau yaliyopita.

Ametamba kwamba atahakikisha anamchakaza Pialali.Naye Pialali amesema kwamba safari hii Mfaume kazi anayo kwamba kichapo atakachokutana nacho sio cha nchi hii.

“Safari hii kazi anayo, huyu ni kondoo sio bondia,” amesema Pialali akimtambia Mfaume.Pambano hilo ni marejeo la pambano lililovufugika Desemba 27 mwaka jana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news