Mama Janeth Magufuli atunukiwa Tuzo ya Heshima nchini DRC

NA MWANDISHI WETU 

MAMA Janeth Magufuli, mke wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa mchango wake alioutoa kwa mwenza wake alipokuwa madarakani.
Tuzo za M. T. KASALU zinatolewa na Taasisi ya LIZADEEL kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya DRC, UNESCO, UN-WOMEN na Asasi za Kiraia. Mama Janeth Magufuli ni miongoni mwa Washindi sita wa Toleo la Tatu la Tuzo hizo zilizokuwa zinawaniwa na wanawake 150.

Washindi wengine ni kutoka nchi za DRC (2), Senegal, Ufaransa na Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Anastahili pongezi Mamaetu, tutamkumbuka sana Hayati JPM

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news