Mradi wa Shule Bora waongeza hamasa Kasulu

NA RESPICE SWETU

WAKATI maafisa elimu awali na msingi wa Hamashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakiwa wanaendelea na ufuatiliaji wa vigezo vya utendaji kazi kwa walimu wa halmashauri hiyo, mradi wa shule bora unaotekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza umeongeza hamasa katika ufuatiliaji huo.
Hali hiyo imetokana na mradi huo kutoa mafunzo kwa wenyeviti wa kamati za shule, walimu wakuu na maafisa elimu wa kata yakiwa na maudhui yanayofanana na vigezo vya utendaji kazi.

Akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo hayo katika Shule ya Msingi Nyakitonto, afisa elimu awali na msingi wa Hamashauri ya Wilaya ya Kasulu,Elestina Chanafi, amewataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo yatakayosaidia kutoa elimu iliyo bora.
Taarifa ya mafunzo hayo iliyotolewa na afisa elimu taaluma wa Hamashauri ya Wilaya ya Kasulu,Joseph Maiga ilisema kuwa, mafunzo hayo ya siku tatu yanayotolewa kwa maafisa elimu wa kata 21, walimu wakuu 85 na wenyeviti wa kamati za shule 85, yalianza Februari 28 na yatafanyika kwa awamu mbili. 

Amefafanua kuwa awamu ya kwanza yenye washiriki kutoka katika kata 14, itakuwa na shule 61 za msingi ambapo awamu ya pili ya mafunzo hayo itakayoanza Machi 7, itawahusisha washiriki kutoka katika kata 7 na shule 24.

Washiriki hao watakaounda ushirikiano baina ya walimu na wazazi (Uwawa) watakuwa na jukumu la kushirikiana katika masuala mbalimbali ya uongozi na maendeleo ya shule.
Mahusiano mengine wanayopaswa kufanyika kupitia ushirikiano huo ni katika uandikishaji wa wanafunzi, kusimamia mahudhurio ya wanafunzi, kukabiliana na mdondoko wa wanafunzi, utoro na kuinua kiwango cha ufaulu.

Masuala mengine ni pamoja na mvuko wa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kwenda sekondari, kusimamia usomaji wa wanafunzi shuleni na nyumbani na kuhamasisha jamii katika kuchangia chakula shuleni. 

Mafunzo hayo yanayofanyika pia kwenye halmashauri za mikoa tisa zinazotekeleza mradi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news