Norway yaahidi mema zaidi kwa Tanzania

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Norway imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ushirikiano katika sekta za kilimo, usalama wa chakula, nishati na mabadiliko ya tabianchi. 
Kikao cha Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen akieleza jambo wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Norway imekuwa mdau mkubwa wa Tanzania katika sekta ya afya na imekuwa ikisaidia katika masuala mbalimbali katika sekta hiyo. 

“Katika hii ziara Mhe. Naibu Waziri anatagemea kufanya ziara ya kutembelea hospitali ya Kiluteri ya Hydom ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali ya Norwa, madhumuni ya zaira hiyo ni kuangalia ni kwa namna gani Norway inaweza kuongeza ushirikiano na kuisaidia hospitali hiyo,” amesema Balozi Mbarouk. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær amesema kuwa ameitembela Tanzania kutokana na ushirikiano imara uliopo baina yake na Serikali ya Norway uliodumu kwa muda mrefu na ulianza kama ushirikiano wa maendeleo. 
“Lengo la ziara yangu hapa Tanzania ni kuangalia ushirikiano katika sekta ya afya kwa sababu Norway imekuwa ikifadhili sekta, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mifuko ya kimataifa, wadau wengine wanaohusika katika sekta ya afya pamoja na asasi za kiraia zinazofanya kazi na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya,” amesema Mhe. Sandkjær. 

Hivyo nitaitembelea Hospitali ya Kilutheri ya Haydom ili kujionea shughuli zinavyofanyika na kuangalia zaidi maeneo ya ushirikiano katika sekta hiyo. 

Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana katika sekta za afya, elimu, uvuvi, nishati jadidifu, kilimo, ushafirishaji na utalii pamoja na masuala ya bahari. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news