Opa Clement wa Simba Queens auzwa Besiktas

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umefikia makubaliano ya kumuuza nahodha wa timu yao ya Simba Queens, Opa Clement kwenda Besiktas ya Uturuki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, tayari mshambuliaji huyo kinara ameshaondoka nchini kuelekea Uturuki kwenda kuanza maisha mapya ya soka katika timu yake ya Besiktas.

Mpaka Opa anaondoka Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) mzunguko wa kwanza umemalizika na yeye ndiye kinara wa ufungaji akiwa amepachika wavuni mabao tisa.

"Uongozi wa Klabu ya Simba unamtakia Kheri Opa katika majukumu yake mapya na pia una mkaribisha muda wowote atakapoamua kurejea tena nyumbani,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news