Rais Dkt.Mwinyi akipa kongole Chama cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA)

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi awapongeza Chama cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA), kwa utaratibu wa kuwaunganisha wananchi kwa kufanya mazoezi kwa kuimarisha afya za watu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na uongozi wa Chama cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) ulioongozwa na Mwenyekiti, Said Suleiman Said (wa tatu kushoto) wakati uongozi huo ulipofika Ikulu jijini Zanzibar hivi karibuni.(Picha na Ikulu).

Sambamba na kuwaweka pamoja, kwani umoja wao unaweza kuleta tija kwa maendeleo katika kuibua fursa mbalimbali kwa vikundi hivyo.

Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo hivi karibuni Ikulu jijini Zanzibar alipokutana na Uongozi wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) , ukiongozwa na Mwenyekiti wake Said Suleiman Said.

Dkt.Mwinyi amesema, hamasa inayotolewa katika ufanyajaji mazoezi ni njia sahihi katika kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni hamasa yenye tija, pia amewaasa kuendelea kuwashawishi wananchi zaidi waendelee kujiunga katika vikundi hivyo walio katika vikundi wasitoke.

Rais Dkt.Mwinyi amewaunga mkono na kuwapongeza kwa utaratibu wa kufanya usafi katika Kisiwa cha Changuu na ameunga mkono wazo la Siku ya Jumamosi kuwa siku ya usafi na ameshauri ili vikundi viwe kimaendeleo zaidi katika uanzishwaji wa shughuli za uzalishaji mali kwa maana inakuwa rahisi kwa Serikali kuwasaidia wakiwa katika vikundi .

Dkt.Mwinyi amewataka ZABESA kushirikiana na sekta binafsi hasa makampuni ya simu na benki kufanikisha matamasha yao kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu ufanyajaji mazoezi na usafi wa mazingira.

Rais Dkt.Mwinyi amewaahidi kushirikiana nao kutafuta waatalamu wa mazoezi ambao watakuwa watajitolea kufundisha vikundi mbalimbali aina za ufanyaji wa mazoezi.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho, Said amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi wake kwa maendeleo anayowaletea Wazanzibari , pia kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar.

Said amesema, wataunga mkono juhudi za Serikali na kubuni miradi mbalimbali mbadala ya kuhifadhi taka.

Alisema, ZABESA imejipanga kuungana na Dunia kuadhimisha siku ya Usafi Duniani inayoadhimishwa kila Jumamosi ya tatu ya mwezi wa Septemba kila mwaka.

Vile vile, wamesema ZABESA ina lengo la kugeuza mtazamo wa kimazoezi na uwe mazoezi kwa afya na maendeleo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news