Rais Dkt.Mwinyi:Lengo la Serikali ni kuimarisha, kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuimarisha na kuweka mazingira mazuri wezeshi ya kibiashara katika uwekezaji hapa nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizindua wa Muongozo wa Uwekezaji Zanzibar na Mfumo wa Kieletroniki wa (ZIPA) uzinduzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Bw.Shariff Ali Shariff.(Picha na Ikulu).

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Machi 10, 2023 katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport jijini Zanzibar wakati akizindua Muongozo wa Uwekezaji na Mfumo wa Kieletroniki wa Uwekezaji (ZIPA).

Dhumuni ni kurahisisha utoaji wa huduma kwa wawekezaji ikiwemo usajili na upatikanaji wa cheti cha uwekezaji wenye jina la"ZANZIBAR INVESTMENT ELECTRONIC WINDOW" (ZieW).
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema kukuza uwekezaji ni moja ya malengo makuu ya Serikali na kuleta Maendeleo.

Amesema, Serikali imedhamiria kuondoa vikwazo vyote vya kisheria na kimfumo vinavyozuia kuwapo kwa mazingira mazuri ya biashara kwa ajili ya uwekezaji nchini.
ZieW unahusisha utoaji wa huduma wa taasisi zote ambazo zipo katika kituo kimoja cha uwekezaji ambapo zitaweza kufanya kazi kwa pamoja na utaruhusu uwepo wa mawasiliano ya pamoja na mwekezaji.

“Kwa kuanzia tayari tumeanza kufanya mabadiliko makubwa ZIPA (Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar) kwa kuimarisha zaidi kituo cha pamoja kutoa huduma za wawekezaji.
"Na jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda ambapo kwa kipindi cha miaka miwili tayari miradi ya 226 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 3.5 ambazo zitatoa ajira 13500 imeanzishwa,”amesema.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema,muongozo wa uwekezaji Zanzibar unaelekeza taratibu zote muhimu za uwekezaji kwa wawekezaji kwa lengo la kukamilisha na kuharakisha usajili wa miradi ya uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amesema, mfumo huo utatoa huduma jumuishi za uwekezaji na nyenzo hizo zitaondoa mianya ya rushwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news