Rais Dkt.Mwinyi:Serikali itatumia matokeo ya tafiti kwa maslahi ya Taifa

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewapongeza familia ya Mama Amne Salim, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Dkt.Salim Ahmed Salim kwa kutoa mchango wao katika kuendeleza tafiti nchini na kuelekeza ufadhili wao.

Lengo likiwa ni kuisaidia Serikali na wananchi wa Tanzania kulielewa janga la Ugonjwa wa Uviko-19. Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Machi 21, 2023 alipofungua Kongamano la Kusambaza Matokeo ya tafiti za Uviko-19, zilizofanywa na Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS).

Ni kupitia mfumo wa ufadhili wa Mama Amne Salim uliyofanyika jengo la CHPE kampasi ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema, taifa bora hujengwa na raia wenye afya, pia kupitia tafiti zinazofanyika hapa nchini kwa kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu changamoto zinazotukabili katika sekta ya afya Serikali upande wa Tanzania bara na Zanzibar ziko tayari kutumia matokeo ya tafiti hizo kwa maslahi ya Taifa.

Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alifarijika kusikia Chuo cha MUHAS kimekuwa cha kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kati kutokana na tafiti, machapisho wanayofanya pia amewaasa kazi zao ziweze kuleta unafuu kwa wananchi kwa kutatua changamoto zinazowakabili katika malengo endelevu.

Pia, alieleza ushirikiano uliopo kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na MUHAS katika kutayarisha mitaala, kusomesha walimu na wataalamu wa afya kwa kuendelea kuimarisha Shule Kuu za tiba na afya ya kinywa.
 
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amewashukuru kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kazi yao katika kuishauri Wizara ya Afya Zanzibar kwa kuunda miongozo mbalimbali kusaidia maboresho Sekta ya Afya Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news