Rais Dkt.Mwinyi:Tatizo la kukosa vipimo sampuli za bidhaa limepata ufumbuzi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussen Ali Mwinyi amesema, Serikali itaendelea kuwalinda wananchi wake kwa kuhakikisha wanatumia bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa nchini zikiwa na viwango vya Kimataifa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Afisa wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) wa Maabara ya Vifaa vya Viwandani,Bi.Sumaiya Ismail Mtoro, wakati akitembelea Maabara Nne Mpya za ZBS baada ya kuzifungua leo Machi 15, 2023 huko Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu).

Mheshimiwa Rais dKT.Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Machi 15, 2023 wakati akizundua maabara nne za Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ambazo vifaa vyake vya kisasa vimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.5.

“Serikali ina nia ya dhati kulinda afya na usalama wa wananchi, kulinda afya zao na kuchukua hatua stahiki bidhaa zinazotumiwa nchini kuwa na ubora unaostahili,”amesema Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Tuzo ya Kuthamini na Kutambua Mchango wako katika kukuza Viwango na Ubora Nchini, akikabidhiwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe.Omar Said Shaban, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maabara Nne Mpya za Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) huko Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja jijini Zanzibar leo.

Maabara hizo na gharama zake ni pamoja na Maabara ya Kemia ya Chakula ambayo imegharimu shilingi milioni 385, umeme shilingi milioni 275, vifungashio shilingi bilioni 2.3 na nguo na ngozi shilingi milioni 600 ambapo Rais Dkt. Mwinyi amesema, tatizo la kukosa vipimo za sampuli za bidhaa limepata ufumbuzi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ZBS, Yussuf Nassor Majid amesema, kupitia maabara hizo watapima bidhaa za chakula, umeme, mafuta nishati, vifaa vya ujenzi hivyo zitaongeza ufanisi na tija.
“Sasa hivi tumewekeza katika maabara zetu za ndani hivyo mapato yaliyokuwa yanakwenda nje yatabaki ndani,” alisema.

Amesema, kuna maabara kubwa ya vifaa vya ujenzi inategemewa kuanza kazi Aprili, mwaka huu ambayo itakuwa na uwezo kupima vifaa vyote vya ujenzi nchini ambayo inagharimu shilingi bilioni 2 ikiwa ni ufadhili kutoka Benki ya Dunia.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban amesema, taifa haliwezi kufanya biashara kama hakuna bidhaa bora, hivyo hatua hiyo inafungua ukurasa wa maendeleo.

Mheshimiwa Shaaban amesema, suala la viwango ni moja kati ya hatua za kuhakikisha wizara inatengeneza mazingira mazuri ya kufanyabiashara nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news