Rais Dkt.Samia aendelea kuifungua Tanzania, Barabara ya Utete-Nyamwage kujengwa kwa lami

NA JOHN MAPEPELE

WAKATI leo Rais wa Jamhuri ya Muungano amepongezwa na Wanawake nchini kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) historia imeandikwa kwa Serikali yake kutia saini mikataba ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage (33.7km) daraja la Mbambe (81m) ikihusisha barabara unganishi (3km) kwa kiwango cha lami.
Barabara hii ni miongoni mwa barabara muhimu kuunganisha mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi na Mtwara.

Mkataba wa leo umeingiwa na Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) na Kampuni ya China Railways Seventh Group Limited.

Aidha, Serikali kupitia wakala huo,imeingia mkataba na Kampuni ya Nyanza Roads Works ,ujenzi wa daraja la Mbambe M81 na barabara unganishi km 3.0 kwa kiwango cha lami , miradi ambayo itagharimu zaidi ya sh.Bilioni 67 hadi kukamilika kwake.
Zoezi la utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa barabara na Daraja hilo, uliofanyika viwanja vya Azimio Utete wilayani Rufiji Mkoani Pwani, umefanyika kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mhandisi Rogatus Matavila pamoja na Mwanasheria wa TANROADS, Dorah Komba ikishuhudiwa na Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa, wananchi, viongozi mbalimbali na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Godfrey Kasekenya.

Mbunge wa Jimbo la Rufiji, ambae pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mohammed Mchengerwa ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Utete-Nyamwage na amewaomba wakandarasi waanze ujenzi kwa kuanzia Utete hadi Nyamwage badala ya kuanzia Nyamwage kwenda Utete.

Amesema wanarufiji wamesubiri kwa kipindi chote ,na Sasa wanaishukuru Serikali kwa maendeleo yanayofanyika na kwamba kukamilika kwa barabara hiyo itasaidia Utete kuwa kitovu Cha maendeleo.
"Walipita viongozi mbalimbali kwa nyakati tofauti,na kila mmoja kuipigania Rufiji kadri ya uwezo wake na leo tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka miwili katuletea neema hii ya barabara ya Utete,"amefafanua Mhe. Waziri Mchengerwa

Tukio hilo limesindikizwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya wilaya ya Rufiji.

Baadhi ya wasanii ambao wamepamba hafla hii ni pamoja na mfalme wa singeli nchini, Sholo Mwamba, Maarifa na Beka Flava.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo , katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) Mhandisi Rogatus Matavila alieleza, mkataba wa barabara ya Utete-Nyamwage ni moja ya mkakati wa Serikali kuharakisha maendeleo ya Rufiji ili kuboresha sekta ya usafiri na usafirishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news