Bodi ya Wakurugenzi ya BoT yafanya ziara TPA, TRC kujionea utekelezaji wa miradi

NA MWANDISHI WETU

BODI ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, imefanya ziara Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kujionea uendeshwaji wa shughuli za kiuchumi na uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta hiyo ya usarifishaji.
Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba, wakitazama reli ya kisasa (SGR) katika stesheni iliyopo jijini Dar es Salaam. 
Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, katika ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyofanyika kwenye bandari ya Dar es Salaam, kujionea namna shughuli za kiuchumi zinaendeshwa katika bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, akifafanua jambo kwa Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyofanyika kwenye bandari ya Dar es Salaam, kujionea namna shughuli za kiuchumi zinaendeshwa katika bandari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Senzige Kisenge, akitoa maelezo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba, kuhusu namna chumba cha uendeshaji kitatumika katika kusimamia kazi za SGR. 
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Senzige Kisenge, akifafanua jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba kuhusu jengo la stesheni ya reli ya kisasa (SGR) lilipo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mrisho S. Mrisho, akifafanua jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba katika ziara ya bodi hiyo ambapo wamejionea namna bandari hiyo inavyoendeshwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news