Kiongozi wa Makuhani Tanzania awatakia Waislamu Eid Mubarak

NA DIRAMAKINI

KIONGOZI Mkuu wa Baraza la Makuhani Tanzania, Master King Prophet John amewatakia Waislamu na Watanzania wote Sikukuu njema ya Eid El Fitr huku akiwaasa kuendelea kudumisha amani, upendo na mshikamano kwa ustawi bora wa Taifa letu.

Master King ametoa salamu hizo Aprili 21,2023 huku akisema ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwajalia ndugu zetu Waislamu kuhitimisha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa amani na furaha.

"Leo ndugu zetu Waislamu wanamaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na kesho (leo Aprili 22, 2023) ni siku ya Eid. Basi nami kama kiongozi Mkuu wa Baraza la Makuhani Tanzania, nimekuja mbele yako ili nimshukuru Mungu kwa upendo na amani ambao ndugu zetu walikuwa wamefunga kwa upendo na amani, tangu siku ya kwanza mpaka siku ya leo wanakwenda kumaliza.

"Basi kwa upendo huu ambao Taifa la Tanzania limejaliwa, tuzidi kuliombea Taifa letu, tusherehekee kwa amani na upendo, tukaribishane, tufurahi sote kwa pamoja ni siku ambayo kiukweli ni siku ya kipekee sana, tuzidi kuliombea Taifa letu la Tanzania lizidi kuwa na amani.

"Tuiombee Serikali yetu, tuwaombee marais wetu, tuwaombee viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mwenyenzi Mungu ailinde na kuliongoza Taifa letu kwa upendo na amani.

"Wakristo wote kwa pamoja, tuwaombee ndugu zetu Waislamu, Taifa letu lizidi kuwa na amani, upendo na mshikamano,What God can do no man can do, Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika Mashariki. Amen,"amefafanua Master King.

Awali Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) lilitangaza sherehe za Eid El-Fitri kitaifa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es Salaam na sala ya Eid itasaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, BAKWATA makao makuu huko Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Pia, sala itaanza saa moja na nusu asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika saa 8 mchana katika Ukumbi wa Kimataifa wa The Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuhudhuria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news