NHC yaanza ujenzi wa majengo ya kitega uchumi Kahama

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi kwa Mkandarasi wa shirika eneo kunapoanza kujengwa majengo ya kitega uchumi yakiwemo maduka, supermarkets, maeneo ya kuoshea magari na maeneo ya huduma mbalimbali za kijamii.
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Shinyanga, Angelina Magazi amesema mradi huo unaoanza unajengwa ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara wilayani humo.

Amesema kuwa, mradi huo utakapokamilika utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania.

Naye Mshauri wa Mradi huo, Godfrey Mkumbo amesema ujenzi wa majengo hayo ya kisasa utakamilika ndani ya miezi sita ukiwa umezingatia viwango vya kisasa.
Mbunifu Majenzi (Arch) Robert Kintu wa NHC (aliyenyoosha kidole) akimwelekeza jambo Mhandisi Mburuga Matamwe (mwenye shati la dtaft) na Godfrey Mkumbo (kushoto) na Mhandisi Masumbuko Majaliwa, wakiangalia ramani ya maduka hayo.

Amesema mradi huo utakuwa na jumla ya maduka 54 yakiwa na huduma zote muhimu za supermarkets, migahawa na maeneo ya kuoshea magari.

Mradi huo unajengwa kwenye eneo la Bukondamoyo mjini Kahama, Shinyanga ilipo stendi mpya ya mabasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news