Simba SC yatembeza kichapo cha mabao 2-0 kwa Yanga SC

NA DIRAMAKINI

KARIAKOO Derby kati ya watani wa jadi Simba na Yanga SC zote za jijini Dar es Salaam, imetamatika kwa Wekundu wa Msimbazi kukomba alama zote tatu huku wakishushia na mabao mawili.

Huu ni ushindi wa aina yake kwa Simba SC kwa kuifunga Yanga katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara,baada ya ushindi wa mwisho wa Februari 16, 2019 ambao waliambulia bao 1-0.

Mwaka huo, Simba SC ilipata ushindi kutokana na bao pekee lililofungwa na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Meddie Kagere ambaye kwa sasa anakipiga Singida Big Stars ya mkoani Singida.

Leo Aprili 16, 2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Simba SC imepata ushindi mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na Henock Inonga dakika ya kwanza na lile la pili Kibu Dennis dakika ya 33. Licha ya Yanga SC kuonesha umahiri ikiwemo kupiga pasi nyingi kulisakama lango la Simba, mabo hayakuwa mazuri kwao.

Aidha, kipindi cha pili Yanga SC walirejea kwa kasi kusaka bao huku Simba wakicheza kwa kujilinda zaidi.

Ushindi huo, unamaanisha Simba SC imefikisha alama 63, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa alama tano na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 26.

Pia, katika mtanage huo, Kipa Ally Salim ni nyota wa mchezo akiwa amelinda lango dakika 90 bila kufungwa katika mtanange huo wa nguvu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news