Tanzania yadhamiria kuyaendea masoko makubwa zaidi duniani

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Tawala Mkoa wa Dodoma, Bw. Ally Senga Gugu amefungua kikao kazi cha kujenga uelewa wa namna ya kupata masoko ya nje kwa wafanyabiashara, viwanda na wazalishaji kilichoongozwa na mshauri mwelekezi wa Kampuni ya Gefrika inayotoa huduma za ushauri wa kiuchumi, Bw. Amine Battikh kutoka Ujerumani.
Gugu amesema, lengo la kikao ni kuweza kutatua changamoto zilizopo ndani ya masoko ya nchini na kuweza kufahamu fursa za masoko ya ndani na nje ya Tanzania na namna ya kuyafikia. Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 27,2023 katika ukumbi wa jengo la Sokoine jijini Dodoma.

"Lengo kubwa tulilopewa sisi ni dhamana ya kufanya kazi na ninyi na kuhakikisha tunatumia ipasavyo fursa za biashara, viwanda na uwekezaji zilizopo jijini Dodoma ambapo ndio makao makuu ya nchi.

"Ikumbukwe kuwa ninyi ndio wakuwafaharisha wanadodoma na Tanzania kwa kuwa mna fursa ya kuwakutanisha na wadau ili kufahamu zaidi kuhusu biashara na kuuza kwenye masoko ndani ya kikanda na kitaifa Tanzania ni nchi ya mwanachama wa jumuiya ya nchi ya Afrika Mashariki tuna hilo soko, lakini bado hatujauza ipasavyo.

"Sisi ni wanachama wa nchi za SADC tunasoko la nchi 15 bado hatujauza vyakutosha, tuna masoko ya kuuza bila kuwekewa ushuru wala kodi, tuna masoko ya umoja wa ulaya ambayo tunatakiwa kuuza kila kitu isipo kuwa silaha. Tunasoko la kuuza China asali, soya na mazao yoyote tunayoweza kuuza lakini hatujaweza kuuza ipasavyo, tuna soko la Uingereza ambayo imejitoa kwenye umoja wa ulaya kwa hiyo tuna fursa ya kutosha,"amesema Gugu.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa Dodoma, Bw.Gugu ametoa rai kwa wafanyabiashara wote kuhakikisha wanatumia fursa hiyo vizuri kwa kuleta matokeo chanya na zoezi hilo la kukaribisha wawekezaji litakuwa endelevu ili kuweza kuendeleza mahusiano mazuri na mataifa mengine.

"Lakini sisi sekretarieti ya Mkoa tutawatengenezea majukwaa kama haya ya kukutanisha na taasisi za umma ili muuze bidhaa zenu lazima mthibitishwe na mashirika ya viwango vya ubora TBS na wengineo, lengo letu ni watanzania kupitia wazalishaji na wafanyabiashara wa Dodoma mtumie fursa ipasavyo ili tuwe na fahari ya kutumia vya kwetu kuuza kwenye masoko ambayo tayari tumesha yapata serikali imefanya jitihada ya kutafuta masoko na hasa soko kubwa ambalo linaitwa 'Afrika Continental Reflected Area.’ Soko huru la biashara Afrika lina watu zaidi ya billioni 1.2 wanaohitaji kutumia bidhaa zetu kwahiyo fursa ni pana,"amefafanua Gugu.

Kwa upande wake Bw. Amine Battikh Mshauri mwelekezi wa kampuni ya Gefrika amesema yuko tayari kuwasaidia wafanyabiashara na wazalishaji hao kwa kuwapatia namna nzuri ya kutatua changamoto zao mbalimbali zinazowakabili kushindwa kufikisha bidhaa kwenye mataifa mengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news