Vigogo wa Serikali wakalia kuti kavu kwa kumtorosha mbakaji Thabo Bester aliyekamatwa nchini Tanzania

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa ameahidi kuchukuliwa hatua kali kwa maafisa kadhaa wa Serikali ambao wanadaiwa kuhusika kutoroka kwa mbakaji wa Facebook,Thabo Bester.

Picha na /Brenton Geach and GoupUp.

Mheshimiwa Ramaphosa pia amesema,Serikali inataka kusafisha mfumo wa haki jinai ili kuhakikisha hakuna aina yoyote ya harufu ya rushwa.

Mhalifu Bester,mpenzi wake Dkt.Nandipha Magudumana na raia mmoja wa Msumbiji kwa sasa wanazuiliwa nchini Tanzania ambapo juhudi za kuwarejesha nchini Afrika Kusini ili kwenda kukabiliana na mkono wa sheria zinaendelea.

Msemaji wa Rais Ramaphosa, Vincent Magwenya amesema Aprili 12, 2023 kuwa, Serikali imefikia uamuzi huo ili kuhakikisha Bester anarudishwa kujibu mashtaka yake kwa madai ya uhalifu.

Amesema, pamoja na kuwa tukio hilo ni la aibu kwa Serikali, vyombo vya sheria viliweza kufanya kazi nyakati zote ili kuhakikisha anakamatwa tena.

"Ilikuwa ni jambo muhimu wale waliokuwa nyuma ya kutoroka kwake (Thabo Bester) kutoka chini ya ulinzi halali wawajibishwe," amesema Magwenya.

Pia amesema,Rais ana uhakika kuwa serikali imefanya kazi kwa bidii kujenga upya mfumo wa haki jinai ili kuhakikisha masuala ya uhalifu yanashughulikiwa kikamilifu.

"Lakini sheria itabidi ichukue mkondo wake, na wale wanaohusishwa na uhalifu uliofanywa na Bester wawajibishwe. Pamoja na kwamba ni aibu, kinachotia moyo ni kwamba bado tuna mfumo imara wa kujibu kwa haraka kesi hizo. Tunao mfumo ambao unaweza kutoa maamuzi haraka, kwani tulishuhudia kwa watu waliokamatwa, na kutakuwa na uwajibikaji kwa sababu uchunguzi unaendelea, na uchunguzi huo utasababisha watu wengi kukamatwa na kusababisha watu wengi kuwajibishwa.

"Katika suala hilo,Rais anasikitishwa na tukio kama hilo, lakini pia anatiwa moyo kwamba vyombo vyetu vya sheria vinaweza kujibu haraka kesi kama hizo. Ni lazima, kwa misingi inayoendelea, kusafisha mfumo wetu, na inazungumza na kazi inayoendelea katika suala la kujenga upya uwezo wa serikali katika ngazi zote na kuhakikisha kuwa tunasafisha mafisadi ndani ya safu yetu ya sheria,"amesema Magwenya.

Ameongeza kuwa, hawawezi kujua ni lini Bester na wenzake watarudishwa kutoka Tanzania kwa kuwa viongozi wa pande zote mbili wako bize na suala hilo.

"Tanzania ina mfumo wake wa kisheria ambao ungehitaji kufuatwa katika kumrudisha mkimbizi kutoka katika haki,"Magwenya amesema huku akibainisha Mheshimiwa Rais Ramaphosa hakutamani tukio kama hilo kuruhusiwa kutokea nchini humo.

Aprili 8, mwaka huu Jeshi la Polisi Tanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram lilisema kuwa,mhalifu wa makosa ya mauaji na ubakaji kutoka Afrika Kusini, Thabo Bester amekamatwa jijini Arusha baada ya kusakwa kwa muda mrefu akiwa na wenzake wawili.

“Ni kweli makachero wetu wamewakamata Thabo Bester, Dkt.Nandira Magudumana na Zakaria Alberto na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.Taratibu za mawasiliano ya kisheria ya ndani na ya Kimataifa zinaendelea kukamilishwa,”ilieleza sehemu ya taarifa hiyo fupi.

Katika hatua nyingine,Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola alisema, Bester alinaswa jijini Arusha Tanzania usiku wa Aprili 7, 2023 pamoja na mpenzi wake wa Afrika Kusini, Nandipha Magudumana na mtu mwingine kutoka Msumbiji.

Naye Waziri wa Polisi nchini Afrika Kusini, Bheki Cele alisema kukamatwa kwa Bester kuliwezekana kupitia ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi la Afrika Kusini, Jeshi la Polisi la Kimataifa (Interpol) na Jeshi la Polisi Tanzania.

"Walionekana wakitoka Dar es Salaam na kufuatwa hadi walipofika Arusha. Ilibainika kuwa walikuwa na hati za kusafiria kadhaa na hakuna hata moja kati ya hizo ambayo imegongwa muhuri nchini Afrika Kusini na Tanzania,"alisema Waziri Cele.

Mbakaji huyo wa Facebook ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela kwa mauaji, alitoroka katika Kituo cha Mangaung huko Bloemfontein mwezi Mei, 2022 baada ya awali kuaminika kuwa alijiua kwa kujichoma moto, ingawa hali ya mashaka ya kifo chake bado ilitanda.(Mashirika/IOL)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news