Waziri Dkt.Chana awapa neno wadau wa michezo, sanaa na utamaduni

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sana na Michezo , Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema, wizara inakaribisha wadau kushiriki katika shughuli za Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwemo matamasha, ligi za michezo mbalimbali katika ngazi zote.
Mhe. Pindi Chana ametoa rai hiyo Machi 31, 2023 jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau tofauti ambapo amesema kuwa, wizara yake inabariki shughuli zote zinazohusiana na Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwataka kuzingatia taratibu, kanuni na miongozo mbalimbali iliyopo nchini.

Wadau hao ni Bw.Japhet Mswaki ambaye ni Mratibu wa Tamasha la Yakwetu Fair Festival, Bw. Rukemo Maasai Muaandaaji wa Tamasha la Maasai Festival pamoja na Bw.Fatih Karakus anayejihusisha na uibuaji wa vipaji vya michezo.

Aidha,Mhe. Balozi Pindi Chana amekutana na Waandaaji wa Tamasha la Pasaka mwaka huu wakiongozwa na Muimbaji wa nyimbo za injili, Christina Shusho ambalo amesema linalenga kuendelea kuhamasisha jamii kushirikiana na kukumbushana upendo, mila na desturi za Kitanzania pamoja na kutoa burudani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news