Wizara ya Maliasili na Utalii yakoleza kasi huku

NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Maliasili na Utalii imeendelea kudumisha ushirikiano na Machifu nchini katika kuhifadhi na kuendeleza urithi wa utamaduni kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ili urithi huo uendane na matokeo chanya ya Filamu ya "The Royal Tour".
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Malikale nchini Dkt. Christowaja Ntandu, alipotembelea Makumbusho ndogo ya Chifu Lazaro Chihoma iliyopo eneo la Kisasa 

Dkt. Ntandu amesema kuwa, Tanzania ina utajiri Mkubwa wa Urithi wa Utamaduni kama inavyosisitizwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa katika adhma yake ya kuhakikisha Wizara inavuka lengo la idadi ya watalii milioni 5 Ifikapo mwaka 2025
Kufuatia hatua hiyo Dkt.Ntandu ametoa wito kwa Watanzania kuanzisha Makumbusho nyingi zaidi ikiwemo Makumbusho za Binafsi pamoja na za Jamii ili kuenzi na kuhifadhi amali adimu zilizopo nchini ikiwa ni fursa ya kuongeza kipato pindi watalii wanapotembelea Makumbusho hizo 
"Lengo la kufika Kwa Chifu Chihoma, kwanza ni kumtambua kama mdau muhimu katika Uhifadhi na Uendelezaji wa Masuala ya Utamaduni wa Mtanzania kwa kuwa na Makumbusho ambayo ni moja ya kivutio muhimu cha Utalii katika Mkoa wa Dodoma," amesema Dkt.Ntandu.
Naye Chifu wa Lazaro Chihoma ameishukuru na kuipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwatambua Machifu nchini kama wadau muhimu katika Uhifadhi wa Urithi adimu wa Utamaduni, na kuahidi kuendelea kutoa mchango wake katika kuhakikisha Makumbusho yake inaongeza chachu katika Uhifadhi, utoaji elimu juu ya utamaduni wa Mtanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news