Alliance in Motion Global yapigwa marufuku Njombe

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, Mheshimiwa Kissa Kasongwa ameisitisha Kampuni ya Alliance in Motion Global inayojishughulisha na uuzaji wa bidhaa za tiba lishe kufanya kazi katika wilaya hiyo.

Ni kutokana na kampuni hiyo kutokuwa na usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),kuwa na uthibitisho mfu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),kutokuwa na TIN Number,kukosa leseni ya biashara pamoja na kukosa utambulisho wa kamati ya ulinzi na usalama.
Mheshimiwa Kissa ametoa maelekezo hayo mara baada ya kupokea taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ambapo pia amebainisha kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikiwapigia simu watu kutoka mikoa mbalimbali kuja wilayani Njombe kwa ahadi ya kupata kazi jambo ambalo limekuwa likiwaumiza vijana wengi kukaa muda mrefu bila kupata kazi baada ya kufika Njombe.

"Akija huku kwa mategemo ya kupata ajira anaambiwa atoe shilingi 30,000 mara toa 600,000 sasa nataka niwaambie Njombe sio shamba la bibi wamekwishatengeneza kelele nyingi na nimepokea watu ofisini kwangu kama mara tatu na kutoa nauli ya watu kurudi Dar es Salaam,kwa hiyo hii kampuni ninaisimamisha kufanya kazi hapa Njombe,irudishe nauli ya watu kurudi kwao,"ameagiza DC Kissa.

Pia, ameitaka kampuni hiyo kufanya kazi kwa kufuata taratibu zote ili kuepusha migogoro inayojitokeza kwa kuwa pia kundi la watu linalodanganywa linaweza kuanza kufanya uhalifu baada ya kukutana na mazingira magumu

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news