Bilionea Rostam Aziz atoa tamko kuhusu mtu anayejiita Kigogo mitandaoni

NA DIRAMAKINI

MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za Taifa Gas,Bilionea Rostam Aziz ameuhakikishia umma wa Watanzania kuwa, hana uhusiano na asingependa kuhusishwa kwa namna yoyote ile na mtu anayejiita Kigogo katika mitandao ya kijamii.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 5,2023 na Ofisi ya Mwenyekiti Mtendaji wa Taifa Group, Bilionea Rostam Aziz jijini Dar es Salaam.
 
"Sambamba na hilo, ndugu Rostam, hakubaliani na tuhuma kadha wa kadha zisizo za msingi wala ukweli ambazo huyu bwana amekuwa akizielekeza kwake binafsi na wakati mwingine kwa viongozi wa Serikali na watu wengine kadhaa.

"Hatua ya mtu huyo, kufuatilia kazi za kampuni yetu ya Taifa Gas na wakati mwingine kupongeza utendaji wake wa kazi haipaswi kuonekana kwamba Taifa Gas inafahamiana naye au pengine kumtumia.

"Ikumbukwe kwamba, wakati fulani mtu huyo huyo alipata kumjeruhi ndugu Rostam na mke wake wakati ule wa mlipuko wa COVID-19 kwa kuandika taarifa ambazo baadaye zilikuja kubainika hazikuwa na ukweli wowote.

"Kwa sababu hiyo basi, mwenyekiti wetu ndugu Rostam Azizi, anawasihi Waatanzania wanaotumia na kufuatilia mitandao kuzingatia misingi ya utu, uwajibikaji na kuwa makini na yale wanayoandika au yanayoandikwa huko. Pia kupuuzia uzushi na uongo unaoenezwa mitandaoni.

"Mara kadhaa kumekuwa na taarifa katika mitandao za kuua na kufufua watu zinazotenegezwa mithili ya hadithi za kufikirika za Alfu Lela Ulela na wakati mwingine kuwatuhumu watu kwa wizi huku wengine wakitengenezwa waonekane ni malaika. Haya ni mambo ya kukemea kwa nguvu zetu zote,"imefafanua kwa kina sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news