ENEO LA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UTENDAJI WA SERIKALI KUJENGEWA UWEZO

NA MWANDISHI WETU

KATIKA kuimarisha Utendaji wa Serikali na Taasisi zake, Serikali ilifanya uamuzi muhimu ya kuanzisha Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wake iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Bunge na Uratibu. Idara hiyo itafanya shughuli zake kwa kushrikisha Wizara, Wakala za Serikali, Idara za Serikali Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa zote.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja kitabu cha tafiti zinazohusu masuala ya Tathmini na Ufuatiliaji, kilichoandikwa na Dkt Steven Masvaure Mtaalam, kutoka katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Johannesburg Afrika ya Kusini baada ya kumaliza kikao kilichoshirikisha, Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali na wataalam kutoka katika chuo hicho.

Hayo yamesemwa mapema leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi alipokutana na Ujumbe kutoka Kituo cha Mafunzo ya Tathmini Afrika (CLEAR-AA) kilichopo katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Johannesburg Afrika ya Kusini na Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali.

Dkt. Yonaz alisema, idara hiyo inategemea kupata ushirikiano kutoka kwa wataalamu mbalimbali ikiwemo kutoka katika Kituo hicho hasa katika eneo la kujengewa uwezo wa ujuzi na utaalamu wa kufanya Tathmini na kuimarisha eneo hilo kwa ujumla. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi akipata maelezo ya moja ya kitabu chenye tafiti za kitaalamu, kuhusu masuala ya Tathmini na Ufuatiliaji, kutoka kwa Dkt. Takunda Chirau Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo na Tathmini Afrika kilichopo katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Johannesburg Afrika Kusini baada ya kumaliza kikao kilichoshirikisha, Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali na wataalam kutoka katika chuo hicho.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja kitabu cha tafiti zinazohusu masualaya Tathmini na Ufuatiliaji, kilichoandikwa na Dkt Steven Masvaure Mtaalam kutoka katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Johannesburg Afrika Kusini baada ya kumaliza kikao kilichoshirikisha, Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali na wataalam kutoka katika chuo hicho.
Washiriki wa kikao cha wataalam kutoka katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Johannesburg Afrika Kusini pamoja na wataalam kutoka Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakifuatilia kikao hicho.

Aliongeza kwa kusema kuwa ni muhimu kufanyika tafiti za kina katika eneo hili ili kuweza pia kurahisisha utekelezaji wake “Pamoja na kuasili kanuni za ulimwengu za Ufuatiliaji na Tathmini katika eneo hili hivyo Tafiti ni muhimu sana,”alisisitiza.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Mafunzo Tathmini na Matokeo Dkt. Takunda Chirau, alisema pamoja na mambo mengine, Kituo hicho kimejikita Zaidi katika Kujenga uwezo wa Tathmini katika Nchi mbalimbali na kufanya tafiti, na kimeshafanya tafiti nyingi katika eneo hili la Ufuatiliaji na Tathmini ambazo pia zinatumika na washirika wa nchi nyingine wanazoshirikiana katika eneo hili.
Mkurugenzi wa Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bi. Sakina Mwinyimkuu katika kikao cha Wataalam kilichohusu masuala ya Tathmini na Ufuatiliaji, Dodoma leo.
Picha ya Pamoja ikimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi (katikati) na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand cha Johannesburg Afrika ya Kusini pamoja na wataalam kutoka Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu.

Awali akiongea katika Kikao hicho Mkurugenzi wa Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bi. Sakina Mwinyimkuu alisema kwamba, Mafanikio ya kuimarisha eneo la Ufuatiliaji na Tathmini yanachangiwa na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali hasa ikizingatiwa kwamba ni eneo mtambuka na linahitaji wadau wengi. 

Hivyo ili kuwezesha utekelezaji wake hakuna budi kuongeza wigo wa wadau kama CLEAR-AA na kuwashirikisha katika kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news