Fei Toto ana kwa ana na Clatous Chama

NA DIRAMAKINI

KIUNGO aliyesusa Yanga, Feisal Salum ameposti picha akiwa na Clatous Chama wa Simba jijini Zanzibar.
Clatous Chama aliyezaliwa Juni 18, 1991 ni mchezaji wa soka wa Zambia ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji wa Simba na timu ya Taifa ya Zambia.

"Unapokuwa Zanzibar na hukukutana na Feisal, basi uko mahali pasipofaa."

Feisal Salum Abdalla, anayejulikana kama Fei Toto amezaliwa Januari 11,1998 ni mchezaji wa soka wa Tanzania ambaye kabla ya kususa alicheza kama kiungo wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania,Young Africans SC.

Aidha,Feisal na Young Africans wana mgogoro wa kimkataba ambapo kiungo huyo inaelezwa alivunja mkataba wake na Wanajangwani hao ili kuwa huru kujiunga na timu nyingine, huku Yanga ikidai bado ina mkataba naye.

Post a Comment

0 Comments