LIVE:Rais Dkt.Samia akishiriki hafla ya kuapishwa Rais mteule Bola Tinubu nchini Nigeria


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Mei 29, 2023 anashiriki Sherehe ya kuapishwa Rais mteule wa Nigeria, Mheshimiwa Bola Tinubu aliyeshinda kiti hicho kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Februari 25, 2023.
Hivi karibuni Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria (INEC) ilimtangaza Bola Tinubu kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais katika uchaguzi uliokumbwa na utata, huku viongozi wa upinzani wakipinga uchaguzi huo kuwa ulighubikwa na utata na kutaka urudiwe mpya.

Tinubu mwenye umri wa miaka 70 na gavana wa zamani wa Lagos anawakilisha chama tawala cha All Progressives Congress, ambacho kilipata karibu kura milioni 8.8 takribani 36.6% ya kura zote, hiyo kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Mahmood Yakubu.

Rais huyo mteule alimshinda makamu wa rais Atiku Abubakar wa chama cha upinzani cha People’s Democratic Party (PDP), na mgombea maarufu wa kikosi cha tatu Peter Obi, ambaye alipata umaarufu miongoni mwa vijana hasa katika hotuba ya kukubalika kwake.

Chama cha upinzani cha PDP kiliyaapuuza matokeo ya uchaguzi huo na kudai uchaguzi mpya kutokana na kile wanachodai kuwa kulikuwa na wizi mkubwa wa kura.

Uchaguzi huo ulikuwa ni miongoni mwa chaguzi zenye upinzani mkali tangu nchi hiyo irejee kwenye utawala wa kidemokrasia mwaka 1999, huku zaidi ya watu milioni 93 wakiwa walijiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa INEC.

Tinubu aliwashukuru wapiga kura na kusema, “Huu ni wakati mzuri katika maisha ya mwanadamu yeyote na uthibitisho wa uwepo wetu wa kidemokrasia. Nawakilisha ahadi na kwa msaada wako, najua ahadi hiyo itatekelezwa,” huku akiwaomba waungane pamoja ili kuimarisha nchi.

Atiku Abubakar, mgombea wa chama kikuu cha upinzani PDP kilichotawala nchi kutoka 1999 hadi 2015 alipata kura milioni 6.9.

Alifuatwa kwa karibu na Peter Obi wa Chama cha Labour (LP), ambaye aliamsha matumaini makubwa miongoni mwa vijana na kukusanya kura milioni 6.1.

Ili kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria, ni muhimu kupata angalau asilimia 25 ya kura katika angalau theluthi mbili ya majimbo 36 ya shirikisho hilo pamoja na eneo la mji mkuu Abuja.

Tinubu gavana wa zamani wa Lagos anamrithi Rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 80 ambaye anajiuzulu baada ya mihula miwili kama inavyotakiwa na Katiba.

Aidha,ikiwa na wakazi wake milioni 216, Nigeria inapaswa kuwa nchi ya tatu yenye watu wengi zaidi duniani ifikapo 2050.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news